Wednesday, April 17, 2013

Gazeti la Mwananchi kuwapa joto wakazi wa MbeyaMuonekano mpya wa Gazeti la Mwananchi

Muonekano mpya wa Gazeti la Mwananchi 

By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Mbeya. Kampuni ya Mwananchi Communications(MCL), leo inaanza promosheni ya kutangaza mwonekane wake mpya wa gazeti la Mwananchi katika Jiji la Mbeya na mikoa yote ya Nyanda za Juu Kusini.


Meneja wa Biashara wa MCL, Bernard Mukasa alisema pia watatumia fursa hiyo ya mpango wa kusambaza magazeti mapema asubuhi katika mikoa ya Kanda ya Kusini.
MCL ni kampuni inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwananchi Jumapili,The Citizen,Citizen On Sunday na Mwananspoti.


Mukasa alisema wataanza promosheni hiyo katika miji ya
Tunduma, Vwawa na Mlolo ambapo watakuwa wakifanya matangazo ya barabarani.Promosheni hiyo itaendelea kesho, Ijumaa itahamia katika Jiji la Mbeya na viunga vyake ambako kutakuwa na shoo kubwa ya burudani.


Mukasa alisema shoo hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Sokoine ikiwashirikisha wasanii maarufu wa muziki wa Bongo Fleva, Profesa J, msanii wa muziki wa taarabu, Snura na Babu Ayubu, ambaye anang’ara katika muziki taarabu pia ni mahiri wa kuiga sauti za watu.


Alifafanua kuwa kiingilio katika shoo kitakuwa toleo la gazeti la Mwananchi au lile la The Citizen la siku hiyo, Aprili 19,2013.“Pia kutakuwa na tafrija itakayofanyika katika Hoteli ya Paradise.


ikihusisha viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mbeya na viongozi wa MCL,” alisema Mukasa, Aliongeza kwamba lengo pia la promosheni ni kusambaza joto la ushindi wa kimbunga, ambao magazeti ya MCL yalipata kwenye tuzo wa uandishi wa hivi karibuni.

-->