#WC2018:, Rivaldo, akiri Brazil, wana, kibarua kigumu Kombe la Dunia

Muktasari:

  • Kikosi cha Tite kinatarajiwa kuingia dimbani leo, kuanzia saa tatu usiku, kuwavaa Switzerland katika mchezo unaotajwa kuwa wa kisasi kutoka na historia ya pande hizo mbili ya miaka tisa iliyopita.

 Moscow, Russia. Endapo watashindwa kutwaa ubingwa wa michuano ya mwaka huu ya Kombe la Dunia 2018, yaliyoingia siku ya nne leo, basi watakuwa wamekwama ndoto zao. Hii ni kwa mujibu wa gwiji wa soka la Brazil, Rivaldo.

Kikosi cha Tite kinatarajiwa kuingia dimbani leo, kuanzia saa tatu usiku, kuwavaa Switzerland katika mchezo unaotajwa kuwa wa kisasi kutoka na historia ya pande hizo mbili ya miaka tisa iliyopita.

Hata hivyo, Rivaldo anaamini kuwa kutokana fomu nzuri walioonesha katika kampeni ya kusaka tiketi ya kwenda Russia, wana kila sababu ya kuwa mabingwa. Samba Boyz, walishindia mechi 17 kati ya 18 walizocheza. Nahodha Neymar anayekipiga katika klabu ya Paris Saint-Germain, aliumia katika kipigo cha 7-1 walichokipata dhidi ya Ujerumani mwaka 2014, lakini atarajiwa kuongoza kikosi watakapowavaa Switzerland, pale Rostov Arena.

  Akizungumzia kikosi cha sasa cha Brazil, Nyota wa zamani wa Barcelona, Rivaldo ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha Brazil, kilichotwaa ubingwa kule Korea Kusini (2002), anasema Wabrazili wanataka ubigwa tu na sio vinginevyo. Rivaldo aliichezea Brazil mechi 75 na kufunga mabao 35. "Kila mara huwa nasema na kusisitiza kuwa, Brazil ni bora.