Zidane ampigia magoti Ronaldo asiondoke

Muktasari:

Ronaldo amekasirika kufuatia madai ya kukwepa kodi inayofikia kiasi cha Pauni 14 milioni na anataka kuondoka nchini Hispania, huku sasa ikidaiwa kuwa na Chelsea na Manchester United zimeingia katika mbio za

 Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amemuomba staa wa klabu yake, Cristiano Ronaldo kuendelea kubaki Santiago Bernabeu licha ya madai ya nyota huyo kutaka kuondoka katika dirisha hili kubwa la majira ya joto.

Ronaldo amekasirika kufuatia madai ya kukwepa kodi inayofikia kiasi cha Pauni 14 milioni na anataka kuondoka nchini Hispania, huku sasa ikidaiwa kuwa na Chelsea na Manchester United zimeingia katika mbio za kumuwania staa huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye kwa sasa yupo Russia akishiriki michuano ya mabara na Ureno.