Kipa mpya Azam aitaka namba ya Manula

Muktasari:

  • Haule amesajiliwa na Azam hivi karibuni akitokea Mbao atakuwa na ushindani na mkongwe Mwadini Ally pamoja na Metacha Mnata, baada ya kipa namba moja Aishi Manula kutimkia Simba.
  • Kipa Haule alidaka kwa kiwango kikubwa msimu uliopita alisema kiwango hakijifichi hivyo atahakikisha anajituma ili kuwa kipa namba moja wa klabu hiyo.

Dar es Salaam. Kipa mpya wa Azam, Benedict Haule amesema atajituma ili kuhakikisha anapata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha mabingwa hao wa Kombe la Mapinduzi.

Haule amesajiliwa na Azam hivi karibuni akitokea Mbao atakuwa na ushindani na mkongwe Mwadini Ally pamoja na Metacha Mnata, baada ya kipa namba moja Aishi Manula kutimkia Simba.

Kipa Haule alidaka kwa kiwango kikubwa msimu uliopita alisema kiwango hakijifichi hivyo atahakikisha anajituma ili kuwa kipa namba moja wa klabu hiyo.

 “Kila sehemu kuna ushindani wa namba, na mpira ni mchezo wa nafasi na kujituma, naamini ukijituma kocha anaona, na hivyo kukupa nafasi ya kucheza na kuonyesha kipaji chako."

“Nimefarijika Azam kwa sababu nimerudi tena nyumbani sehemu ambayo nilikuwepo zamani, hivyo kitu ninachowaahidi mashabiki nitajituma kwa uwezo wangu wote ili kuing'arisha timu hii kwenye ligi msimu ujao," alisema Haule.

Haule alisema kama wachezaji wote wa kikosi hicho wakijituma anaamini timu hiyo itachuku ubingwa msimu ujao.

“Mashabiki watarajie mazuri zaidi, tutajitahidi kwa nguvu zote,  kwa uwezo wetu wote, tutajituma tuhakikishe tunaiwezesha timu kutwaa bingwa na kushiriki mashindano ya kimataifa msimu ujao," alisema  Haule.