Mpenzi wa Wedd kuchezesha Bundesliga

Muktasari:

Mwanamama huyo mwenye miaka 38 na ofisa wa polisi wa Hanover, ambaye ni mpenzi wa mwamuzi wa zamani wa England, Howard Webb, ametangazwa na Shirikisho la Soka Ujerumani jana kama mmoja wa waamuzi wanne wapya watakaochezesha msimu ujao.

Bibiana Steinhaus ametajwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa mwamuzi katika historia ya Ligi Kuu Ujerumani (Bundesliga).

Mwanamama huyo mwenye miaka 38 na ofisa wa polisi wa Hanover, ambaye ni mpenzi wa mwamuzi wa zamani wa England, Howard Webb, ametangazwa na Shirikisho la Soka Ujerumani jana kama mmoja wa waamuzi wanne wapya watakaochezesha msimu ujao.

Steinhaus alikuwa mwamuzi wa Ligi Daraja la Kwanza (Bundesliga 2) tangu 2011, pia akiwa mshindi wa tuzo ya mwamuzi bora wa mchezo wa soka kwa wanawake kati ya Japan na Marekani kwenye fainali za Olimpiki mjini London 2012.

"Wakati Lutz Michael Frohlich (Mkuu wa Kamati ya Waamuzi ya Ujerumani) aliponitaarifu, nilikosa neno la kusema," alisema Steinhaus alipozungumza na mtandao wa DFB.

"Nilihisi kama sitaki kuamini, furaha ilizidi, nikapata ahueni, ilikuwa ni hali ambayo hakika siwezi kuielezea!

"Haikuwa ndoto yangu hasa kuwa nitakuwa mwamuzi wa Bundesliga. Lakini tukio hili limekuja moja kwa moja katika kiwango changu cha mwisho cha furaha."