Simulizi ya mwanafunzi aliyepigwa risasi na polisi

NIT, WANAFUNZI WAMZUNGUMZIA AKWILINA ALIYEUAWA NA POLISI

Muktasari:

Daladala hilo linaonekana limejaa, hakuna siti yoyote, lakini msichana huyo hakujali, aliingia kwenye basi hilo na kusimama, safari ikaanza.


Saa 11 jioni maeneo ya Mabibo jijini Dar es Salaam, msichana mrembo na anayejiamini anaingia kwenye basi la daladala huku simu yake ikiwa sikioni akizungumza na mtu mwingine.

Daladala hilo linaonekana limejaa, hakuna siti yoyote, lakini msichana huyo hakujali, aliingia kwenye basi hilo na kusimama, safari ikaanza.

Alikuwa anakwenda Kijitonyama ili awahi mabasi ya kwenda Bagamoyo, lakini safari yake ikaishia njiani.

Safari yake ikaishia njiani mara mbili; hakufika Kijitonyama alikokuwa anakwenda, lakini pia safari yake ya duniani ikawa imeishia hapo.

Hiyo ni safari ya mwanafunzi wa shahada ya kwanza wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwiline aliyeuawa juzi kwa kupigwa risasi na polisi, ambaye simulizi yake imewekwa kwenye gazeti la Mwananchi la Jumapili. Usikose kupata nakala yako.