Monday, March 20, 2017

Asilimia 96 ya wanawake waofanya kazi sokoni hunyanyaswa

 

By Ephrahim Bahemu, Mwananchi ebahemu@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Ofisa Mwezeshaji kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake (WLAC), Jane Majijita  amesema asilimia 96 ya wanawake wanaofanya biashara sokoni na asilimia 40 ya walio katika mahusiano hufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia.

Amesema hayo mwishoni mwa wiki alipotoa mada kwa wakazi wa Kata ya Makuburi iliyopo Manispaa ya Ubungo ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa kituo hicho kutoa elimu ya kisheria na kijinsia.

Majijita amesema takwimu zilizotolewa na Taasisi ya Equity For Growth (EFG) mwaka 2009 zinaonyesha asilimia 44 ya wanawake wote nchini wamepitia unyanyasaji wa kijinsia, hivyo ni suala la kupingwa kwa nguvu.

“Tatizo la unyanyasaji wa kijinsia bado ni kubwa, hata sisi tunaojitahidi kupambana nalo tunakutana na changamoto ya takwimu kwa sababu Serikali ilitoa agizo kwamba takwimu zote zitoke katika mamlaka zilizothibitishwa kuzikusanya lakini mambo mengine tunayashuhudia ndiyo maana tunatafuta namna ya kuwasemea watu,” amesema Majijita.

-->