#WC2018: Brazil yapewa nafasi kutwaa taji Kombe la Dunia Russia

Muktasari:

Historia inaonyesha kwamba ni kazi ngumu kwa timu ambayo imetwaa taji hilo kulitetea kwa sababu kila baada ya miaka minne huibuka wachezaji chipukizi kwenye timu za taifa ambao wanakuwa tishio kwenye mashindano hayo.

Russia. Ujerumani inapewa nafasi finyu kutetea taji lake la ubingwa kwenye Kombe la Dunia Russia kutokana na historia ya fainali hizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930.

Historia inaonyesha kwamba ni kazi ngumu kwa timu ambayo imetwaa taji hilo kulitetea kwa sababu kila baada ya miaka minne huibuka wachezaji chipukizi kwenye timu za taifa ambao wanakuwa tishio kwenye mashindano hayo.

Katika historia ya mashindano hayo ni nchi mbili pekee ambazo zilifanikiwa kutetea mataji yao ya Kombe la Dunia. Brazil ilichukua mfululizo mara mbili mwaka 1958 na mwaka 1962. Pia Italia ilifanya hivyo mwaka 1934 na mwaka 1934.

Lakini jambo la kusikitiza Italia haipo kwenye fainali za mwaka huu kutokana na kushinda kufuzu.

Hata hivyo, Brazil ya miaka minne iliyopita inaonekana imepiga hatua zaidi kwa sasa, ambapo kikosi chake kinaonekana kuwa moto wa kuotea mbali. Hivyo ni  miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi kubwa zaidi kulinyakua taji hilo.