DAWALISHE: Ulaji wa fenesi husaidia kutibu ngozi iliyojikunja

Fenesi ni miongoni mwa matunda  yenye ladha tamu linalotajwa kuwa na faida nyingi mwilini. Miongoni mwa faida zake ni kuongeza ufanisi wa mfumo wa kinga mwilini, kuongeza kinga dhidi ya kifua, mafua na kikohozi kutokana na kuwa na vitamini za aina mbalimbali.

Kutokana na faida zilizopo katika tunda hilo, huna sababu ya kuacha kulila tunda hili ambalo linanunuliwa na wengi kutokana na kupatikana maeneo mengi.

Wataalmu wa  afya wanaeleza kuwa ,Fenesi lina fibre inayosaidia kulainisha choo pamoja na virutubisho vingi kama vitamini A, C, B complex, vitamin B6, folic acid, niacin, riboflavin na madini ya aina mbalimbali ambayo ni potassium, magenesium, manganese na chuma.

Mbali na vitamin zilizopo katika Fenesi, tunda hili lina  protini, mafuta, wanga na antioxidants huku  likitajwa kuwa chanzo kizuri cha nishati kisichokuwa na mafuta.

Ulaji wa fenesi mara kwa mara  huzuia kansa na kutibu seli zilizoharibiwa na kansa pamoja na magonjwa yanayotokana na uharibifu wa mazingira.

Pia, hutibu magonjwa ya moyo, tatizo la damu na hulinda ngozi.

Madini  kama  magnesium na kalisiam yaliyopo katika fenesi husaidia kuimarisha mifupa hivyo ulaji wa tunda hili mara kwa mara hutibu magonjwa ya meno na mifupa ambayo ni dhaifu, huku Vitamin C iliyopo katika tunda hilo likifanya kazi nzuri katika uimarishaji wa meno.

Vilevile, hulinda ngozi zilizojikunja na hii ni kutokana na kuwa kiasi kikubwa cha mafuta ambayo husaidia kulainisha ngozi na kuipa muonekano unaong’aa.

Ulaji wa fenesi mara kwa mara huyawezesha macho kuwa na uwezo mzuri wa kuona, kuondoa  ukosefu wa choo, kuondoa gesi tumboni na kutibu vidonda vya tumbo.

Faida nyingine ni kukabili tatizo la kuwahi  kufika kileleleni kwa wanaume nja kukosa hamu ya tendo kwa wanawake.

Fenesi hurekebisha msukumo wa damu, hurahisisha mmeng’enyo wa chakula tumboni na kuukinga mwili dhidi ya magonjwa ya moyo na kupooza.

Hata hivyo, ulaji wa gramu 100 za fenesi huweza kuupatia mwili nguvu ya kalori 95 huku sukari aina ya fructose na sacrose iliyomo ikiupatia mwili nguvu.