Monday, March 20, 2017

DC Nyamagana awaangukia wajasiriamaliMkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha. 

By Juma Ng’oko, Mwananchi mwananchipapers@mwananchi.co. tz

Mwanza. Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha amewaomba msamaha wajasiriamali wadogo walioathiriwa na operesheni ya kuwaondoa katikati ya jiji, akisema alifanya hivyo kutetea ajira yake.

Amesema hayo wakati akifunga mafunzo ya ujasiriamali na kuzindua kampeni ya elimu kwa jamii wilaya za Nyamagana na Ilemela jijini hapa.

“Ndugu zangu, siyo kwamba mimi nilipenda ama nilipata faida kuwaondoa kwa nguvu katikati ya jiji; la hasha, nilifanya hivyo kulinda mkate wangu,” amesema.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Dk Leonard Masale aliwapongeza waliofuzu mafunzo hayo, huku akisema watapewa kipaumbele na halmashauri wakati wa kukopesha asilimia 10 ya fedha zitokanazo na mapato ya ndani. 

-->