MAGONJWA NA TIBA: Maambukizi ya bakteria na tiba kwa wanawake

Muktasari:

Leo nitaeleza hatua za kuchukua ili kupambana na maambukizi haya, kupunguza ukali wake ukishapata na hata kuzuia yasijirudie baada ya tiba.

Maambukizi ya bakteria sehemu za siri za mwanamke ni moja ya magonjwa  yanajitokeza kwenye afya uzazi  mara kwa mara. Pamoja na kuwapo kwa msaada kutoka kwa wahudumu wa afya, lakini hata mwanamke mwenyewe anaweza kujipa huduma za awali hata akiwa nyumbani ili kukabiliana na tatizo lenyewe. Takwimu zinaonyesha mwanamke mmoja kati ya wanne wana maambukizi ya bakiteria. Baadhi yao hawaoni dalili zozote wakati tatizo hili linapowapata hadi pale linapodumu kwa muda mrefu ndipo wanaweza kuona dalili ya muwasho ukeni, kutokwa na ute mzito ukiambatana na harufu kali.

Baadhi ya dawa za kiantibayotiki zinasaidia kuponya tatizo hili, japo kwa wengine tatizo hili hujirudia mara kwa mara hata baada ya kutumia dawa, kuto.

Leo nitaeleza hatua za kuchukua ili kupambana na maambukizi haya, kupunguza ukali wake ukishapata na hata kuzuia yasijirudie baada ya tiba.

Kwanza mgonjwa anapaswa kujua wakati upi ni sahihi wa kumuona daktari. Ndani ya uke kuna uwiano kati ya bakteria na fangasi.

Bakteria na fangasi hawa waliopo ndani ya uke hawana madhara kiafya kama wapo kwenye uwiano sawa.

Lakini inapotokea idadi ya kundi moja linazidi lingine, ndipo maambukizi hayo huanza. Hata hivyo, mtu anaweza kupona kwa kutumia baadhi ya antibayotiki, lakini pia unashauriwa kumuona daktari haraka kama ni mjamzito.

Maambukizi ya hayo wakati mwingine ni ishara kuwa mimba inaharibika au unaweza kuzaa kabla ya wakati, kuzaa mtoto mwenye uzito mdogo na matatizo mengine ya ujauzito.

Ni muhimu kumuona daktari kwa wakati huo kuliko kutumia dawa za kawaida kwa sababu haziwezi kuwa msaada stahiki kwa mjamzito.

Tofauti na ujauzito, pia unaweza kuona ishara ya maumivu makali wakati wa kukojoa, kutokwa damu wakati ambao haupo kwenye mzunguko wa hedhi, na maumivu kwenye njia ya mkojo, homa, maambukizi kujirudia hata baada ya kutumia dawa, yanaweza kuashiria tatizo zaidi.

Ni vema kumuona daktari. Utafiti wa kisayansi unathibitisha matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango mathalani ile ya kuwekwa kitanzi inachangia maambukizi hayo kutokana na utokwaji wa damu ambao mara nyingi hufululiza kwa muda baada ya kuwekewa kitanzi. 

Hivyo daktari anaweza kuamuru kukitoa  na kushauri kutumia njia nyingine ya uzazi wa mpango.

Pili, unapaswa kujua kuwa kufanya ngono kunasababisha maambukizi haya ya bakiteria.

Maambukizi hayo  yanaweza kuambukizwa kama magonjwa mengine ya zinaa, ni vema kwa mwanamke kujiepusha na ngono isiyo salama hadi hapo maambukizi yatakapotoweka baada ya tiba.

Kufanya ngono mara kwa mara na hasa na watu tofauti, kunaweza kuvuruga uwiano wa bakteria asilia walioko kwenye sehemu za siri na hivyo kusababisha maambukizi mapya. Lakini unaweza kujikinga na hili kwa njia zifuatazo.

Epuka kufanya ngono mara kwa mara na hasa  kwenye njia ya haja kubwa kwa sababu kufanya hivyo unachanganya uchafu wa njia ya haja kubwa na wale bakteria asilia wa ukeni. Pia ni vema kutumia dhana za kuzuia maambukizi wakati wa kufanya ngono kama vile kuvaa kondomu. Na pia unashauriwa kwenda kukojoa mara tu baada ya kufanya ngono. Baada ya kukojoa jisafishe vizuri kwa maji safi.

Tatu unashauriwa  kuvaa na kutumia vifaa vinavyoendana na afya ya uke. Kwa sababu maambukizi ya bakiteria yanaweza kukusababishia kutokwa na harufu mbaya.

Maswali na majibu piga na sms kwa simu: 0658 060 788