Riba za benki kikwazo mikopo ya ujenzi wa nyumba

Muktasari:

Shirika la Mikopo ya Nyumba (TMRC), lilianzishwa kwa lengo la kuziwezesha benki kutoa mikopo  kwa wateja ambao wana lengo la kumiliki nyumba za kudumu.  TMRC inaendeshwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kumilikiwa na Benki ya CRDB, NMB, Exim, Azania, DCB na NIC ambazo kila moja ina hisa zinazozidi thamani ya Sh500 milioni.

WAKATI likihimiza makazi bora kwa kila mwananchi kwa sababu ni sehemu ya haki za msingi za binadamu, mataifa mbalimbali yanajitahidi kufikia lengo hilo.

Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimeridhia maazimio mbalimbali ya Umoja wa Mataifa likiwamo Azimio la Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa (UN-Habitat).

Moja ya maazimio ya UN-Habitat ni kutaka wananchi kuwa na makazi bora na shirika hilo limekuwa likitekeleza mpa ngo wa mikopo ya nyumba kwa wanajamii.

Mikopo hiyo ni aina ya huduma ambayo hutolewa na taasisi za fedha katika nchi nyingi kote duniani, ikiwa na lengo la kuwajengea wananchi uwezo wa kumiliki nyumba za makazi au biashara.

Hivi karibuni kutokana na ma badiliko ya kiuchumi, Tanzania imeingia kwenye biashara hiyo hasa baada ya wananchi na taasisi zake kuwekeza katika eneo hilo.

Ili kufanikisha mpango huo, Benki Kuu ya Tanzania (BOT), imetoa kibali cha kuanzishwa kwa shirika ambalo litazijengea benki zetu uwezo wa kutoa mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya manufaa kwa wananchi.

Shirika la Mikopo ya Nyumba (TMRC), lilianzishwa kwa lengo la kuziwezesha benki kutoa mikopo  kwa wateja ambao wana lengo la kumiliki nyumba za kudumu.  TMRC inaendeshwa na kusimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kumilikiwa na Benki ya CRDB, NMB, Exim, Azania, DCB na NIC ambazo kila moja ina hisa zinazozidi thamani ya Sh500 milioni.

Lengo la TMRC kuwa chombo cha uhakika cha kusimamia mikopo ya muda mrefu ya benki, kuweka mazingira ya kuwapo kwa  riba nafuu, kupunguza ukomo wa kurejesha mikopo na kutoa mikopo  kwa wateja wanaokidhi vigezo na masharti.

Wastani wa kiwango cha chini cha riba, Novemba mwaka jana ni asilimia 16 wakati kiwango cha juu ni asiliamia 26. Kiwango cha riba kinatofautiana na aina mkopo na benki.

Shirika hilo lina wanachama 11 ambao ni Benki za CRDB, NMB, DCB,  Banc ACB, NIC, TIB, Exim, PBZ, Azania, BOA na NBC. Kutokana na kuwapo kwa mpango huo Benki ya Azania imenufaika na mkopo baada ya kupata Sh4.2 bilioni. Taasisi hiyo inatarajia kujiendesha kwa kuuza zabuni katika soko la hisa na  kuzikopesha kwa benki kwa utaratibu maalumu. Mteja atapata mkopo kutoka benki, ambayo itakopeshwa na TMRC wakati yenyewe ikipata fedha kutoka soko la hisa.

Kuwapo kwa chombo kama TMRC kutawezesha  kuanzi shwa kwa kampuni binafsi ya kutoa mikopo ya nyumba kama ambavyo imefanyika katika nchi nyingine duniani ambako biashara hii imeshamiri kwa kiwango kikubwa. Nchini Misri kampuni nne binafsi zilianzishwa baada ya kuwapo kwa Shirika la Mikopo ya Nyumba mwaka 2006 na ku sababisha mapinduzi makubwa katika sekta ya nyumba na makazi. Maonyesho ya nyumba yameanza kufanyika ili kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali kupata fursa za kuwekeza katika biashara hiyo.

Katika maonyesho yaliyofanyika kwa mara ya pili mwishoni mwa mwaka jana, wadau tofauti walipata nafasi ya kujifunza mambo mengi kuhusu nyumba na uendeshaji wa biashara. Baada ya shirika hilo kuanza kazi, mabadiliko yameanza kujitokeza katika soko kwani benki kadhaa zimeanza kutoa mikopo ambayo imekuwa ikiwaumiza wananchi wengi kutokana riba kubwa inayotozwa.

Riba kubwa imekuwa ki kwazo kwa wananchi wengi na kusababisha Rais Kikwete kuziomba taasisi hizo kupunguza riba ya mikopo ili kuwapa nafuu wananchi wengi. Kaimu Mkurugenzi TMRC, Oscar Mgaya, anasema ili kuleta ushindani zaidi katika soko ni vyema benki nyingi zikashiriki mpango huo.  “Benki nyingi zaidi zinatakiwa ama ziruhusiwe au zishiriki katika mpango huu wa kutoa mikopo ya nyumba ili kuongeza ushindani sokoni na kupunguza kiwango cha riba kwa wakopaji.

Tangu kuanzishwa kwa shirika hilo karibu miaka miwili iliyopita, kumekuwa na msukumo mkubwa kwa benki katika kutoa mikopo ya nyumba.

Ofisa Habari wa Benki ya Azania, Rhino Nyansaho ana sema mpaka sasa benki hiyo imetoa mikopo ya zaidi ya Sh111 bilioni kufikia Desemba 2012 kwa wateja zaidi ya 4,000.

Naye Ofisa Uhusiano wa Benki ya Boa Patricia Nguma, anasema wana karibu mwaka mmoja tangu waanze kutoa mikopo nyumba ambayo  inafikia Sh3 bilioni kwa  wateja 20.

Mikopo inayotolewa kwa shilingi ya Tazania riba yake ni zaidi ya asilimia 18 wakati inayotolewa kwa dola ya Marekani inaanzia asilimia 9 na kwamba mabadiliko yanatokana na tofauti ya thamani ya fedha hizo katika masoko.

Kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa Watanzania wana nia ya kumiliki nyumba na kuwa na makazi bora lakini riba ni tatizo kubwa ambalo inawaondoa katika uwezekano wa kuwa wamiliki.

Moja ya sababu ya benki kutoza riba kubwa inaelezwa kuwa ni kuporomoka mara kwa mara kwa shilingi ya Tanzania.

Hali hiyo  inasababisha upatikanaji wa mikopo ya nyumba kuwa mgumu na   kuonekana kuwa ni kwa ajili ya watu wenye kipato kikubwa.