Christopher Mwahangila, Goodluck Gosbert na Rehema Lupilya wachuana vikali

Sunday November 19 2017

 

Wimbo mpya wa Mungu Hawezi Kukusahau wa mwimbaji mkongwe wa muziki wa injili nchini, Christopher Mwahangila umeshikilia chati katika orodha ya nyimbo kumi bora zilizofanya vizuri mwezi Septemba, mwaka huu.

Nafasi ya pili imechukuliwa na wimbo mpya wa ‘Mwema’ kutoka kwa mwimbaji mchanga Rehema Lupilya wakati nafasi ya tatu ikiangukia kwa mwanamuziki nyota, Goodluck Gozbert na wimbo wake mpya wa ‘Wastahili Sifa’ .

Katika orodha iliyoachiwa kwenye mtandao wa gospomedia.com unaofanya kazi chini ya Kampuni ya Gospo Media nyimbo za waimbaji hao zimepata watazamaji na wasikilizaji wengi katika mwezi huo mara tu baada ya kutua sokoni.

Akizungumza na Mwananchi, Mkurugenzi wa Gospo Media, Ladslaus Milanzi alitaja nafasi ya nne kuwa imeshikiliwa Judith Mbilinyi ‘Maisha Yangu’, Stanley Qamara ‘Jinsi Ninavyokupenda’ Matto Cole ‘Grown’ na Andrew Robinson ‘ You are God’.

Nyimbo nyingine mpya zilizofanya vizuri ni kutoka kwa Voniyke kutoka nchini Nigeria umeshika nafasi ya nane, Nakupenda kutoka kwa Benny William na Back To You kutoka kwa mwimbaji na rapa T Babz wimbo Back To You.

Alisema waimbaji wengi wa muziki wa injili wanafanya kazi nzuri na kwamba orodha iliyoachiwa ni ya nyimbo mpya na kwamba, hizo tatu zimesikilizwa zaidi ikilinganishwa na nyingine kwa mwezi huo.

“Muziki wa Injili kwa sasa upo kwenye mchuano mkali kwa sababu waimbaji ni wengi na wanafanya kazi nzuri sana, hii inaonyesha kuwa kazi ya Mungu inazidi kusonga mbele,” alisema.

Alisema orodha hiyo huwa inaandaliwa kila mwezi kulingana na namna kazi mpya za wasanii zilivyopokelewa sio tu kwenye mitanda

Mwahangila alisema katika wimbo wake mpya uliofanya vizuri amewashirikisha kundi la kusifu na kuabudu la The Sauti Light Worshippers la jijini Dar es Salaam.

“Namshukuru Mungu kwa sababu wimbo huu unafanya vizuri, na kila nilipoenda watu wameupokea vizuri kama ule wa Mungu ni Mungu,” alisema.

Kwa upande wake Judith Mbilinyi alisema kazi nzuri ya muziki inahitaji kujituma na kwamba, anashukuru kuingia kumi bora.

“Namshukuru Mungu kwa sababu na ni mwanamuziki mchanga lakini, kazi yangu imefanya vizuri. Asante wadau walionipokea,” alisisitiza.

Advertisement