Icheki, hii hapa First 11 ya Wekundu wa Msimbazi

Muktasari:

2- Shomary Kapombe

Alianzia katikati ya msimu na katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar ambayo walishinda mabao 2-0. Tangu hapo amekuwa mchezaji wa kutumainiwa kikosi cha kwanza.

1- Aishi Manula

Hakuna ubishi, ndiye mchezaji aliyecheza mechi nyingi mpaka sasa katika kikosi cha kwanza cha Simba. Amecheza mechi 28 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 13. Haitashangaza mwisho wa msimu kutajwa kipa bora.

2- Shomary Kapombe

Alianzia katikati ya msimu na katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Kagera Sugar ambayo walishinda mabao 2-0. Tangu hapo amekuwa mchezaji wa kutumainiwa kikosi cha kwanza.

3- Asante Kwasi

Simba wamemsajili katika dirisha dogo akitokea Lipuli ya Iringa. Ameongeza nguvu kwa kiasi kikubwa akifunga mabao mawili. Kikubwa ni kuwa ana namba yake kikosini.

4- Erasto Nyoni

Amesajiliwa na Simba msimu huu akitokea Azam. Amekuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza na licha ya kucheza nafasi ya beki ameifungia timu yake mabao matatu muhimu moja dhidi ya Yanga juzi tu hapa.

5- Yusuph Mlipili

Msimu wake wa kwanza Simba, alisajiliwa akitokea Toto Africans ambayo ilishuka daraja. Hakuwa na msimu mzuri chini ya Joseph Omog, alikuwa hapati nafasi lakini kuondoka kwa kocha huyo kumemfungulia njia.

6- Jonas Mkude

Kama Mlipili, hakuwa akipangwa sana chini ya Omog, lakini tangu alipoondoka, mambo yakanyooka na amecheza mechi 20 akiwa katika kikosi cha kwanza na ndiye mhimili.

7- Nicholas Gyan

Amesajiliwa na Simba akitokea nchini Ghana mwanzo wa msimu kama fowadi, lakini tangu alipokuja kocha Pierre Lechantre amekuwa akimtumia kama mlinzi wa kulia.

8- James Kotei

Kiungo Mghana wa Simba nae aliongeza mkataba wa miaka miwili mwanzo wa msimu na ameendelea kusalia katika kikosi cha kwanza kwa kuonyesha ubora wake.

9- John Bocco

Straika aliyesajiliwa akitokea Azam msimu huu. Amekuwa na maelewano makubwa na Emmanuel Okwi na peke yake amefunga magoli 14 yaliyosaidia kuipa ubingwa.

10- Emmanuel Okwi

Kinara wa mabao katika Ligi Kuu Bara. Amefunga magoli 20 na amekuwa na mchango mkubwa katika timu na wakati mwingine akikosekana, mbele kunapwaya na iko hivyo.

11- Shiza Kichuya

Winga na kiungo wa Simba, amefunga mabao saba katika Ligi Kuu Bara anongoza kwa kutoa pasi za mwisho akiwa ametoa pasi 17 nyingi kuliko mchezaji yoyote katika Ligi.