Friday, July 21, 2017

JEURI YA MAYWEATHER: Amwambia McGregor, we maskini tu

 

LONDON, England. Floyd Mayweather jeuri sana aisee. Pesa aliyo nayo ndiyo inampa ujeuri. Unajua hii ikoje, juzi alimwambia mpinzani wake, McGregor, “Wewe masikini tu.”

Mabondia hao wako kwenye kulinadi pambano lao na juzi walikuwa SSE Arena kwenye Uwanja wa Wembley, na katika tambo zao, Money Man alimwambia mpinzani wake, Conor McGregor “Wewe ni masiki tu na hunifikii kwa fedha.”

McGregor hakuwa na cha kusema zaidi ya kucheka na kujitetea akisema subiri ulingoni.

Mayweather alimwonyesha saa yake na kumwambia: “Ushahidi wa kwanza kuwa wewe ni masikini ni saa uliyovaa. Wewe ni masikini ndio maana unavaa saa za bei rahisi.”

Bondia huyo ilibidi anywee kwani wakati akisema hayo, alikuwa akimwonyesha saa yake iliyotengenezwa kwa vito vya almasi aina ya Hublot ikiwa na thamani ya Dola 1.4milioni (Sh3,136bil), na alikuwa akimwonyesha mara kwa mara.

Akizungumza baada ya kupewa kipaza sauti, Mayweather alimwambia McGregor: “Wewe ni mtu mwepesi, angalia.”

Bondia huyo alinunua saa hiyo Hublot alipokuwa katika matembezi Dubai mwaka  2015 na amekuwa akiivaa mara kwa mara katika matukio muhimu.

Si kwa saa tu, bondia hiyo ambaye amepigana mara 40 na hajawahi kupigwa amekuwa akivaa shingoni vito vya thamani na mkononi pia. Pia anautajiri unaofikia Dola550milioni.

Bondia hiyo anatarajia kuingoza Dola78m akipambana na McGregor mpambano utakaofanyika T Mobile Arena mjini Las Vegas Agosti 26.

-->