KILIMO CHA KISASA: Kanuni za 5 muhimu za kufanikiwa katika kilimo biashara

Upandaji: Kutumia mbegu au kuandaa kitalu kutokana na aina ya mbegu.

Muktasari:

>Uchaguzi wa mbegu

>Kutoa katika kitalu hadi shambani

>Uwekaji mbolea

>Unyunyizaji wa dawa

>Kuweka maji katika mmea kwa wakati maalumu

>Kuthibiti wadudu na magonjwa

>Kukomaa kwa matunda na mboga

>Uvunaji mazao

>Utayarishaji wa mazao kwa mauzo ama kuhifadhi

Upandaji wa mazao ya kibiashara haswa  mboga na  matunda katika hapa Tanzania unazidi kuwa mkubwa sana na watu wengi sana wanaendelea kuingia katika kilimo.

Imeshakuwa kama ada vile mkulima mmoja akivuna akapata pesa wenzake humtumia yeye kaka mfano na wao kuingia katika kilimo kwa kukurupuka.

Mwishowe hupata hasara kubwa sana na kumwona Yule aliyemshawishi aingie katika kilimo ni muongo. Leo napenda kuchukua fursa hii katika ukurasa wetu huu kuwapa wakulima elimu kubwa sana ambayo naamini kuwa kama kila mjasiriamali ataifuata elimu hii hatojuta katika kilimo chake hasa mazao haya ya matunda na mboga mboga.

Napenda kuyasema hayo kwa sababu bidhaa au mazao yanayopatikana katika kilimo tunachofanya huuzwa katika masoko ya humu nchini na mengine soko la nje.

Ni muhimu kutaja hapa kwamba wanunuzi na walaji wa mazao na bidhaa zinazotokana na mazao haya wanazidi kuwa waangalifu na huzingatia ubora wamazao wanayopata kutoka kwa soko.

Kwa sababu hii basi, mkulima anapaswa kuzingatia kanuni 5 zifuatazo hasa kabla hawajakurupuka na kuingia katika kilimo biashara.

Njia ya kwanza ni kukuza mimea

Ni muhimu kwa mkulima kujiuliza je, katika msimu huu ni mmea gani ninastahili kupanda? Bila shaka mkulima anapaswa kufanya uamuzi kuhusu mmea au mimea atakayopanda na kukuza.

Ni vyema basi mkulima afanye makadirio ya gharama za mimea anayotarajia kupanda na kutambua faida kutokana na mimea hii mbalimbali hii itapatikana kwa kuandaa mpango kazi niliouelezea wiki iliyopita.

Akishatambua ni mimea gani anapanda na kukuza ni muhimu pia kuangalia mambo yafuatayo:

Aina gani au ni shina mama lipi litakalotumika wakati wa kupanda Ubora wa mbegu Kinga dhidi ya wadudu na magonjwa

Pili ni wakati wa kupanda

Kwa mkulima anayechukulia kilimo kama biashara, ni muhimu ajiulize je, ni wakati gani wa kupanda? Kwa wakulima wengi jawabu linalokuja kwa fikra zetu mara moja ni wakati wa mvua. La hasha! Wakati mzuri wa kupanda unatambulika vyema tunapozingatia mambo fulani katika soko kama vile:-

Ni wakati au muda gani mmea wako utakomaa?

Wakati uhitaji (demand) wa zao uko juu pale ambapo bidhaa huwa adimu sokoni.

Wakati bei ya mazao ni nzuri kwa mkulima.

Wakati utoaji (supply) wa zao uko chini kabisa.

Ni muhimu kwa mkulima kuwa na muongozo wa upandaji mazao yake na vizuri zaidi akatushirikisha wataalamu na pia wakati huo huo awe ameshadadisi uhitaji wa mazao sokoni.

Tatu ni mahali pa kukuza

Mimea huleta mazao mazuri na mengi hasa unapopandwa eneo ambalo kitaaalamu udongo wake utalandana na zao hilo. Hivyo mkulima aidha aupime udongo wake au aulizie historia ya eneo hilo analotegemea kwenda kupanda mimea yake. Kuchunguza eneo kutasaidia kupata taarifa pia ya wadudu wasumbufu na wanyama pia. Lakini pia kuyajua magonjwa hatarishi kwenye eneo husika. Inasikitisha sana kuona mkulima anaotesha mbegu zake kisha akija anakuta wanyama kama panya wameshazitafuna. Hii inatokea sana na hivyo kumpotezea mkulima malengo yake na humletea gharama. Haya yotr hutokea kama mkulima hatoifanyia kazi  kanuni ya kuchagua mahali sahihi pa kukuzia mmea wake.

Lakini pia mkulima anapaswa kujihakikishia kuwa mvua ikinyesha mazao yake yatakuwa salama katika eneo hilo.

Anapaswa kuhakikisha kuwa panapitika hasa kipindi cha mvua na kipindi cha kawaida. Tumeona juzi tu mvua hizi zilivyonyesha wakulima walikimbia mashamba yao na mashamba mengine tayari yalikuwa na mazao ya kuvunwa lakini miundo mbinu ni mibovu ya kuelekea shamba. Hii ikapelekea mazao kuharibika.

Hiyo haitoshi eneo la kilimo linapaswa kuwa na usalama kwa binadamu na mazao. Kwa sababu utaweka vijana wa shamba waishi hapo. Mwisho kabisa maji yawepo, bila maji kilimo hakiwezi kwenda. Na kama hamna je una uhakika upi ukichimba kisima hutokumbana na chumvi kali ambayo kwa kilimo haitofaa?

Ndo mana kama mtalaamu nitakushauri leo ndugu mkulima kuwa bora ukanunua shamba lenye gharama kubwa sana lenye miundo mbinu muhimu yoote muhimu kwa ajili ya kilimo lililo jirani na maeneo ya barabara, mjini au sokoni au karibu na maji kuliko kununua shamba la bei nafuu mahala ambapo hamna maji, hapapitiki, kuna wanyama wakali. Mara nyingi rahisi rahisi huwa kwa ujumla naweza nikasema kuwa ni muhimu kufahamu kwamba kila mmea una mahitaji tofauti kwa kukua vyema.

Hivyo nisisitize kuwa mkulima ni lazima azingatie haya kwenye eneo hilo:-

Udongo: Udongo wa eneo hilo ni sharti ufanyiwe utafiti na kufahamika wazi aina, upungufu wake, na sifa zake muhimu.

Mvua: Mvua inayopatikana katika eneo hili ni muhimu kujulikana, kama ni viwango vyakutosha au la.

Joto: Mimea ni lazima ikuzwe katika maeneo yenye joto kulingana na mahitaji ya mmea.

Upandaji na ukuzaji

Katika kilimo cha biashara ni muhimu kuzingatia mambo yafuatayo:-

Utayarishaji shamba: Shamba ni sharti zitayarishwe ipasavyo kwa kuchimbua kikamilifu, kuondoa manyasi, magugu hatari na kuinua mchanga kimo cha sm 5. Kwa kuboresha mazao na wingi wake, ni muhimu mkulima atumie mbinu zilizo na gharama ya chini lakini apate faida kubwa. Basi mkulima inapaswa awe na utaalamu wa kilimo katika mambo yafuatayo:-

Na tano ni wateja

Wateja wa kisasa hujali sana ubora wa mazao na afya zao. Ni muhimu kwa mkulima kutambua mahitaji na matakwa ya wateja wake kabla ya kupanda na kutunza mimea yoyote.