Friday, July 21, 2017

Kocha Wenger Kaanza mapema, autaka ubingwa

Arsene Wenger akizungumza na wachezaji wake

Arsene Wenger akizungumza na wachezaji wake wakiwa Austria kwa mechi za maandalizi. 

Inawezekana ana kumbukumbu ya mabango ya mashabiki uwanjani, inawezekana ana kumbukumbu ya maandamano ya kutaka ang’olewe na inawezekana pia anakumbuka ndege zilizokuwa zinapita juu ya utosi wake zikiwa na mabango yanayomtaka aondoke.

Pamoja na hayo, kikubwa zaidi, inawezekana pia Wenger nafasi aliyoshika ya tano katika msimamo na kumkosesha Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza, pengine ndiiko kulikomfanya aanze na tizi la kufa mtu.

Kikosi cha Arsena kimeanza ziara ya mbali, kimetua Australia na baadaye ziara ndefu ya China kabla ya kurudi London kwa ajili ya michuano ya Emirates Cup ambayo inafanyika London na Arsenal ni mwenyeji.

Michuano ya Emirates inashirikisha timu zote zinazodhaminiwa na Emirates mbali na Arsenal, ni pamoja na AC Milan, Real Madrid, Paris Saint-Germain. Emirates walianza kuidhamini Arsenal 2004.

Katika ziara yake hiyo ya pre-season, Arsenal itakuwa Australia na China ikiwa ni maandalizi ya Ligi Kuu msimu wa 2017-18 na pia itatoa nafasi kwa mchezaji mpya, Alexandre Lacazette ambaye atakuwa katika fulana ya Gunners kwa mara ya kwanza.

Lacazette ameungana na Sead Kolasinac katika kikosi hicho cha London na kutengeneza ladha kwa ajili ya msimu ujao.

Ilivyo sasa

Australia wataipokea Arsenal. Watacheza mechi mbili kwenye mji wa Sydney dhidi ya timu za A-League, Sydney FC waliyoichapa 2-0 na Western Sydney Wanderers na mechi zote zitachezwa kwenye Uwanja wa ANZ wenye uwezo wa kuchukua mashabiki  83,500. Uwanja huo ulitimika kwa Michezo ya Olimpiki mwaka 2000.

Baada ya mechi hizo, itasafiri kwa saa 10 kuitafuta Shanghai, China, watakakocheza na Bayern Munich kwenye Uwanja wa Shanghai.

Baada ya mchezo huo, timu itasafiri kwenda Kaskazini mwa Beijing kucheza na Chelsea, ni kama mechi ya Ngao ya Hisani, kwani itacheza na Chelsea Julai 22. Mechi hiyo itachezwa Uwanja wa Bird’s Nest – Uwanja ulioandaa Michezo ya Olimpiki 2008.

Arsenal ambao ni mabingwa wa FA watacheza na bingwa wa Ligi Kuu, Chelsea Agosti 6 kwenye Uwanja wa Wembley.

Baada ya hapo, timu itarejea London kwa ajili ya michuano ya Emirates Cup na kabla ya mashindano, itakuwa na mechi mfululizo.

The Gunners itajigawanya mara mbili na itakwenda kucheza na Benfica na Sevilla, pamoja na RB Leipzig imealikwa kwenye mashindano lakini haitacheza na Arsenal.

Ozil: Nitabaki Arsenal

Kumbe zilikuwa mbwembwe za kutingisha ili aonekane naye yupo, Mesut Ozil amesema kuwa anataka kubaki Arsenal wakati mwenzake, Alexis Sanchez amebakishwa kusubiri warudi kwani alikuwa kwenye Kombe la Mabara na Chile.

Pamoja na kwamba timu nyingine za Ligi Kuu England zitakuwa muda mwingi ugenini, Arsenal itatumia muda mwingi London, kushir

-->