Magufuli atamudu ukongwe wa kisiasa wa CCM?

Rais John Magufuli

Muktasari:

Julai 23, CCM watafanya mkutano wao mjini Dodoma maalumu kwa ajili ya kumkabidhi kijiti cha uenyekiti wa chama, Rais John Magufuli ili awe mwenyekiti wa tano wa chama hicho kikongwe nchini.

Hakuna ubishi kwamba ukivitazama vyama vya kisiasa vinavyotawala nchi kadhaa barani Afrika kwa kipimo cha ukongwe, Chama cha Mapinduzi (CCM) kinazidiwa na ANC cha Afrika ya Kusini pekee.

Ukongwe wa chama ni tatizo? Kimsingi kila chama kina muda wa uhai wake na hata wanachama wapo hai na wale wasiokuwa hai.

Ni wazi kuwa ukongwe wowote ule uwe wa mwanadamu au mashine huendana na matatizo ya ukongwe huo. Kwa chama cha siasa, ukongwe unaweza kuwa katika sura mbili, wa wanachama au umri wa chama.

Kuhusu wanachama, kama chama kitashindwa kuzalisha wanachama vijana asilimia kubwa ya wanachama wake huwa wazee hivyo kukosa nguvu kutoka kwa vijana.

Kwa bahati nzuri vyama makini vya siasa kama CCM vililijua hili mapema ndiyo maana vina jumuiya za vijana, wanawake na wazee ambayo hujulikana kama jumuiya ya wazazi ya CCM.

JPM atakaposhika uenyekiti wa CCM atakuwa anashika uenyekiti wa moja ya vyama vikongwe vya siasa barani Afrika. Historia yake kisiasa haionyeshi kama amepitia ukada wa chama ingawa hilo siyo tatizo kwake.