Mbappe ananunua wachezaji hawa 11

Muktasari:

Mkataba uliomalizika mwaka jana haufikii wachezaji 11 ambao wote kwa pamoja thamani yao haifikii thamani ya usajili wa kumtoa Mbappe klabuni hapo.


Manchester City imekuwa kwenye mbio za kumnyakua mchezaji huyo nyota wa raia wa Ufaransa, lakini pia timu hizo zinazomuwania zinapaswa kujitahadhari kutokana na wakati mwingine kujikuta wakiwekeza nguvu nyingi kwenye usajili ghali kwa mtu mmoja.

Mkataba uliomalizika mwaka jana haufikii wachezaji 11 ambao wote kwa pamoja thamani yao haifikii thamani ya usajili wa kumtoa Mbappe klabuni hapo.

1. Kipa, Jasper Cillessen (Pauni 11 milioni)

Kipa huyo anayedakia Barcelona na timu ya Taifa ya Uholanzi, alihama kutoka Ajax msimu uliopita kwa uhamisho wa Pauni 11 milioni.

Alitwaa mataji mawili akiwamo medali kwenye mashindano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2014.

Amekuwa kipa tegemeo katika kikosi cha Barcelona msimu huu na anafahamika zaidi kwa jina la Jasper.

2.Beki wa kulia, Thomas Munier ( Pauni 5 milioni)

Ni raia wa Ubelgiji mwenye miaka 25, anacheza beki ya kulia. Alichukuliwa kutoka klabu ya PSG msimu uliopita wa kiangazi kwa thamani ya Pauni 5 milioni kwenda klabu ya Brugge.

Mchezaji huyo amekataa ofa ya kucheza Ligi ya England badala yake ametua Ufaransa ambako anakipiga kwenye Ligi

        3.Beki wa kushoto, Raphael Guerreiro (Pauni 10 milioni)

Dotmund ndiyo walioula kumsainisha mkataba mchezaji huyo. Unaweza ukasema ni mkataba mnono kwake.

Mchezaji huyo mzaliwa wa Ufaransa mwenye uraia wa Ureno, alijiunga na kikosi cha Thomas Tuchel baada ya kutia saini mkataba wa thamani ya Pauni 10 milioni wakati wa msimu wa kiangazi mwaka 2016.

Katika Ligi hiyo ya Bundesliga, amecheza michezo 16 akifumania nyavu mara nne, huku akiwa ametoa mapande matano yaliyozaa mabao.

4. Beki wa kati, Florian Lejeune (Pauni 1.5 milioni)

Lejeune (25) aliondolewa Manchester United alikokuwa anasugua benchi na kujiunga na Basque wakati wa msimu wa kiangazi na akachomoza kwenye La Liga na alijiimarisha zaidi akiwa kama beki wa kati hatari.

Mlinzi huyo ana umbo kubwa lililokwenda hewani, kuna taarifa za kuwapo machakato wa kurejea katika Ligi Kuu ya England kwenye klabu ya Arsenal au Tottenham msimu ujao. Dau lake kumng’oa katika klabu hiyo inaweza kuongezeka zaidi ya kiwango alichosajiliwa awali.

5. Beki wa kati, Antonio Rudiger (Pauni 7.5 milioni)

Mchezaji mwenye asili ya Ujerumani lakini baba na mama yake ni raia wa Sierra Leone. Rudiger alichomolewa Stuttgart na kwenda Roma msimu uliopita wa kiangazi. Mchezaji huyo awali alitokea kwenye kituo cha vijana cha michezo cha Dortmund na hivi sasa yupo chini ya kocha Luciano Spalletti.

Rudiger, kwa sasa ni mchezaji wa kimataifa wa Ujerumani na hivi karibuni amekuwa akihusishwa kuhamia klabu za England hususan Chelsea na Liverpool.

6. Kiungo wa kati, Idrissa Gueye (Pauni 7 milioni)

Ligi Kuu ya England ina mtu anayeitwa, Gueye anayechezea Everton. Unaweza kusema ndiye N’Golo Kante mpya raia huyo wa Senegal. Wote kwa pamoja wamesajiliwa England ndani ya msimu mmoja lakini yeye ni mkongwe kuliko nyota huyo wa Chelsea.

Wakati macho yote yakiwa kwa Romelu Lukaku ambaye anatarajiwa kuondoka msimu huu kurudi Chelsea, kuna Guaye ambaye naye ni kati ya mafundi wa soka katika klabu hiyo.

7. Kiungo wa kati, Victor Wanyama (Pauni 11 milioni)

Ni vigumu kuamini kwamba ni mmoja wapo wa wachezji wa Ligi Kuu anayeweza kumeza thamani ya mchezaji mmoja. Mchezaji huyo wa Tottenhm ana thamani ya Pauni 11 milioni na ndiyo imetokea kwa Mbappe thamani yake kuweza kuunganisha na kupata kikosi kizima.

8. Kiungo wa kati, Marcelo Brozovic (Pauni 4 milioni)

Mchezaji huyo ni miongoni mwa chipukizi ambao wanaonekana kutisha kwenye safu ya kiungo. Mchezaji huyo raia wa Croatia alijiunga na Inter Milan akitokea Dynamo Zagreb mwaka 2015 kwa mkopo.

Hata hivyo, amejihakikishia namba kwenye kikosi hicho kwenye msimu wa kiangazi akiikaribia thamani kwa asilimia 4.4 ya mchezaji ghali Paul Pogba.

Amecheza mechi 17 za Ligi Kuu katika msimu huu akirekebisha makosa yake ya awali na kuhimili mikiki ya bosi wake mpya, Stefano Pioli.

9. Kiungo mshambuliaji, Serge Gnabry (Pauni1 milioni)

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 21 alikuwa kimya kwa takriban mwaka mzima. Gnabry ametokea Arsenal akiwa mchezaji wa kimataifa na mfungaji mahiri wa ‘hat trick’.

Hat trick yake ya kukumbukwa aliipiga wakati timu yake ilipokutana na San Marino, hata hivyo amepelekewa kwa mkopo West Brom.

10. Kiungo mshambuliaji, Ousmane Dembele (Pauni 12.5 milioni)

Dembele ataweza kujilinganisha ubora wake na Mbappe katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali mechi itakayocheza Aprili.

Dembele raia wa Ufaransa, amekuwa akifananishwa na mshambuliaji huyo wa Monaco kwa kuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaochipukia Ulaya.

Aliwahi kushinda ubingwa wa Ligue 1 na kutangazwa kuwa mchezaji chipukizi kwa mwaka 2016. Aliwahi kuingizwa kati ya orodha ya wachezaji bora 50 akishika nafasi ya nane katika uchambuzi wa Gazeti la Daily Mail.

11. Straika Monalo, Gabbiadini (Pauni 14.5 milioni)

Straika wa Southampton, ameshuka kiwango chake tangu alipotua Napoli mwezi Januari.

Mchezaji huyo raia wa Italia amefanikiwa kushinda kwenye michezo saba aliyopangwa uwanjani akiwa Seria A. Pia akiwa kwenye maisha mapya ya soka England, alishinda mara mbii Kombe la EFL wakati timu yake ilipokutana na Manchester United kwenye fainali.

Wachezaji wote hao thamani yao jumla yake inafikia Pauni 88 milioni.