Utatu Mtakatifu- Hakuna tena kama ilivyokuwa MSN

Muktasari:

  • Ulaya nzima, hakuna kilichokuwa kinapingana na hiki kifupi, ‘MSN’.

Ulaya nzima, hakuna kilichokuwa kinapingana na hiki kifupi, ‘MSN’.

Katika Ligi ya Mabingwa, klabu inayopangiwa na Barcelona, akili ya kwanza ni kwa Messi, Suarez na Neymar. Hakuna tena utatu kama huo, lakini sasa umesambaratika.

Barcelona ilitwaa ubingwa ikiwa na MSN, ilinyanyasa klabu za dunia ikiwa na MSN, lakini sasa nguvu yake imemeguka.

Imekwanyuka kwa kuwa Neymar katimkia Paris Saint-Germain kwa dau kubwa, Euro 466 milioni ambako huko sasa wanataka kutengeneza utatu wao matata Neymar, Edinson Cavani na Kylian Mbappe.

Wafuatao ni wachezaji wanaotengeneza utatu katika klabu zao kwa sasa, ukiacha MSN ambayo imepanguka.

REAL MADRID: Karim Benzema, Gareth Bale, Cristiano Ronaldo.

Tangu Gareth Bale ajiunge na Karim Benzema, Cristiano Ronaldo mwaka 2013, maswali mengi yaliibuka kuhusu safu ya ushambuliaji Real Madrid itakuwa katika ubora gani.

Ronaldo amekuwa katika ubora wake muda mrefu na mabao yake yamekuwa yakichagizwa na Benzema wanaocheza pacha katika safu ya ushambuliaji.

Hata hivyo, safu imekumbwa na maswali mengi kuhusu uwezo wao wa kufunga mabao kwa kuwa imekuwa ikimtegemea zaidi Ronaldo ingawa huwezi kumbeza Benzema na Bale.

BARCELONA: Lionel Messi, Luis Suarez, Ousmane Dembele

Licha ya kumkosa Neymar, lakini safu ya ushambuliaji Barcelona ni moto wa kuotea mbali kwa kuwa bado Lionel Messi yuko kwenye ubora wake.

Mpaka sasa, Messi amefunga mabao 11 katika mechi saba zamwanzo na anatarajia kuendeeleza moto huo. Pia Luis Suarez bado ana kiwango bora.

Barcelona imeongezewa nguvu na kinda wa miaka 20 Ousmane Dembele ingawa winga huyo wa Ufaransa ameanza vibaya baada ya kupata majeraha yaliyomuweka nje mapema.

PSG: Kylian Mbappe, Edinson Cavani, Neymar.

Paris Saint Germain inatajwa kuwa ndiyo timu yenye washambuliaji watatu mahiri duniani. Ikitumia fedha nyingi kunasa saini zao.

Timu hiyo inapewa nafasi ya kutwaa ubingwa wa Ufaransa baada ya kunasa saini za Mbappe, Neymar na Messi.Licha ya kuibua mzozo na Edinson Cavani, wachezaj hao wakuwa tishio katika safu ya ushambuliajiwakiongozwa na Mbappe.

Haitakuwa ajabu kwa miamba hiyo ya soka Ufaransa kutwaa ubingwa msimu huu kutokana kwa mahasimu wao Monaco.Harry Kane, ameiteka dunia baada ya mabao yake kuing’arisha Spurs na tayari ameanza kufananishwa na wachezaji nyota Lionel Messi au Cristiano Ronaldo.

Akicheza mbele ya kiungo nyota duniani, Dele Alli, 21, Kane ameanza kuwa gumzo Spurs. Pia Christian Eriksen, 25, amekuwa chachu ya mafanikio.

Kane aliyepewa kitambaa cha unahodha wa England, anatarajiwa kung’ara msimu huu na ameingia katoka orodha ya wafungaji bora England.

MAN CITY: Gabriel Jesus, Sergio Aguero, Raheem Sterling.

Man City inaongoza Ligi Kuu England kutokana na safu yake ya ushambuliaji kuwa imara na kuzipiku timu zingine ikiwemo Manchester United.

Timu hiyo inapambwa na washambuliaji watatu wakali Sergio Aguero aliyefunga mabao sita nyuma Romelu Lukaku, licha ya kucheza dakika chache 163.

Mbali na Aguero, Man City inatambia Raheem Sterling mwenye mabao matano na Gabriel Jesus manne. Timu hiyo ina straika wengine hodari David Silva, Leroy Sane Bernardo Silva.

MAN UNITED: Marcus Rashford, Romelu Lukaku, Juan Mata

Jose Mourinho ana kikosi bora cha ushambuliaji hakuna ubishi, ana kila kitu. Romelu Lukaku, haraka amekuwa tegemeo Man United akiwa amefunga mabao 11 katika mechi 10.

Marcus Rashford ni mchezaji mwenye kipaji na chipukizi akishambulia kutoka kushoto pembeni mwa uwanja, wakati Juan Mata ni hodari akitokea upande wa kulia.

Man United ina muungano mzuri kutoka kwa viungo Henrikh Mkhitaryan anayecheza nyuma yao. Baada ya kumkosa Zlatan Ibrahimovic, Man United imelamba dume kwa kupata saini ya Lukaku.

CHELSEA: Alvaro Morata, Pedro, Eden Hazard

Edin Hazard ameanza msimu mpya vibaya baada ya kushindwa kutamba kutokana na majeraha hatua ambayo ilimkosesha amani kocha Antonio Conte wa Chelsea.

Ingawa Hazard amerejea uwanjani hivi karibuni, bado hajaanza kufanya vitu vyake na ni mchezaji tegemeo wa Chelsea.

Hata hivyo, Conte ana mbadala Chelsea Alvaro Morata aliyemsajili majira ya kiangazi kutoka Real Madrid baada ya kubaini udhaifu katika safu ya ushambuliaji.

Morata raia wa Hispania ameanza kuwa gumzo, baada ya kucheza kwa kiwango bora katika michuano tofauti ikiwemo Ligi Kuu England.

Mhispania huyo anatajwa kuwa na uwezo mzuri wa kufunga na akicheza na Pedro atajenga muungano mzuri wenye tija kwa Chelsea katika michuano mbalimbali.

LIVERPOOL: Roberto Firmino, Mohamed Salah, Sadio Mane, Philippe Coutinho

Kocha Jurgen Klopp hana shida ya kusaka namba tisa bora katika kikosi chake msimu huu kwa kuwa ana straika wa ukweli wenye uwezo mkubwa duniani.Salah, Firmino na Mane wamekuwa wakifanya kazi nzuri Liverpool ingawa wameshindwa kufunga mabao mengi katika Ligi Kuu England.

Mbrazil Coutinho amekuwa chachu ya mafanikio Liverpool akicheza nyuma yao akiwa chanzo cha mashambulizi ndani ya kikosi hicho.

Pamoja na kushindwa kutamba, lakini Liverpool imeingia katika orodha ya washambuliaji nyota wenye uwezo mzuri wa kufunga mabao.

Wakati Mane ni hodari wa kufunga mabao, Coutinho ni hodari wa kuanzisha mashambulizi ndio maana Barcelona hadi leo wanalia naye kutoka saini yake muda mrefu.

BAYERN MUNICH: Robert Lewandowski, Arjen Robben, Thomas Muller

Tangu alipojiunga na Bayern Munich akiwa mchezaji huru kutoka Borussia Dortmund, Lewandowski ameipa ubingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu Ujerumani chini ya kocha Jurgen Klopp.

Lewandowski amefunga mabao 30 katika misimu kadhaa yakiwemo matano aliyofunga ndani ya dakika tisa katika mchezo wa ligi akitokea benchi dhidi ya Wolfsburg mwaka 2015.

Pia huwezi kumuweka kando mkongwe Arjen Robben kwa kuwa Mholanzi huyo ameonenyesha bado ana kiwango bora cha kutisha duniani.

Mbali na kina Lewandowski, Bayern Munich inatambia Franck Ribery na James Rodriguez ambao wamekuwa chachu ya m mafanikio katika kikosi hicho kutoka Makao Makuu Allianz Arena.

JUVENTUS: Mario Mandzukic, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala.

Juventus haiko nyuma katika safu ya ushambuliaji, ina straika hodari wenye majina makubwa wanaotamba Ulaya na miongoni mwao ni Mario Mandzukic, Gonzalo Higuain na Paulo Dybala.

Mandzukic na Higuain wamekuwa katika kiwango bora na nwamekuwa hodari wa kufunga mabao katika timu hiyo maarufu m‘Kibibi Kizee’ cha Turin.

DORTMUND: Andrej Yarmolenko, Pierre-Emerick Aubameyang, Christian Pulisic

Baada ya mshambuliaji nyota Marco Reus kupata majeraha, Dortmund ina mchezaji mwenye nguvu na akili anayeweza kuziba vyema pengo hilo ambaye ni Andrej Yarmolenko.

Yarmolenko anaweza kucheza vyema katika safu ya ushambuliaji akicheza na Pierre-Emerick Aubameyang, Christian Pulisic anayetokea pembeni.

Nyota hao watatu na Maximilian Philipp, wametengeza pointi 15 za Dortmund na kupata mabao 21 katika Ligi Kuu Ujerumani msimu huu.

Kwa wastani wa wachezaji watatu katika kila mchezo, wamelingana na Manchester United na kuingia katika rekodi ya kuwa moja ya timu bora Ulaya.

ARSENAL: Alexandre Lacazette, Mesut Ozil, Alexis Sanchez

Katika miaka mitatu iliyopita Arsenal haikuwahi kuwa na washambuliaji nyota wanaoweza kubadili sura ya mchezo au kuwa tishio dhidi ya mabeki wa timu pinzani.

Lakini kocha Arsene Wenger, amekuna kichwa na kupata safu imara ya ushindi baada ya kuvuna straika watatu mahiri kina Alexandre Lacazette, Mesut Ozil na Alexis Sanchez.Ingawa Ozil anacheza nafasi ya kiungo mshambuliaji, lakini mchango wake wa kulisha mipira kwa kina Lacazette na Sanchez umekuwa na manufaa msimu huu katika Ligi Kuu England. Ozil anatajwa ni mchezaji mjanja mwenye uwezo wa kuchezesha timu, Sanchez ana nguvu na Lacazette ni hodari wa kumalizia mipira.