Young Killer ajiapiza kuwa hawezi kufulia

 Young Killer Msodoki  ni miongoni mwa wasanii walioibuka miaka ya hivi karibuni walioleta upinzani katika muziki wa Hip Hop nchini.Hivi karibuni alizua sintofahamu baada ya kutoa wimbo Sinaga Swaga uliopokelewa kwa hisia tofauti.

 Wengine wanausifu wimbo huo kwamba unaonyesha ni kiasi gani amepevuka, wengine wanaubeza kuwa ni wa kujikweza katika hadhi ambayo hajaifikia na kwamba anaanza kupotea katika muziki.

Nini utafanya ukifulia kimuziki?

Mimi nafanya muziki kwa ajili ya kuburudisha watu sio kushindana. Siamini kama nitafulia kiasi kwamba hakutakuwa na Mtanzania hata mmoja anakayetaka kusikia kazi zangu; kwahiyo kama nitapotea sitaacha muziki, nitajitahidi kufanya kwa ajili ya hao wachache waliobaki na uhitaji wa kunisikia.

Ukipewa nafasi uchague mmoja awe mpenzi wako kati ya Wema Sepetu na Zari, utatoka na yupi?

Sidhani kama naweza kuchagua. Zari na Wema wote ni wanawake wazuri, wanavutia na nawapenda. Kama kuna uwezekano nipewe nafasi ya kuchagua kuwa nao wote wawili.

Una jozi  ngapi za viatu na ni kipi cha gharama ndogo zaidi?

Nina kama jozi 30 za viatu; na kuhusu bei mimi sichagui, navaa kiatu hata cha bure ilimradi kiwe na muonekano unaotakiwa.

Kiasi kikubwa cha pesa ulichowahi kumuhonga mwanamke?

Sikumbuki kama nilishawahi kuhonga na kama nimewahi basi itakuwa ni vocha ya buku.

Kwenye video ya nyimbo yako mpya unaonekana umevaa pete nyekundu, ina maana gani?

Haina maana yoyote, niliivaa tu ili mikono yangu isiwe mipweke na ndiyo maana leo unaniona sina pete.