Arsenal yarudi mtaa wa saba tena!

Muktasari:

  • Kocha wa West Ham, David Moyes ajiwekea rekodi ya kutofungwa kwenye mechi mbili za Chelsea na Arsenal.

Suluhu ya Arsenal dhidi ya West Ham imeirudisha tena kwenye nafasi ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu England.

Mchezo huo uliopigwa jana Jumatano usiku ulimuwezesha kocha David Moyes kuweka rekodi ya kutofungwa kwenye mchezo wa pili hadi sasa.

Mshambuliaji wa Arsenal, Jack Wilshere licha ya kurudi dimbani hakuweza kuzifumania nyavu, huku suluhu hiyo ikiipelekea Arsenal hadi nafasi ya saba.

Kwa maana hiyo, Arsenal itakuwa chini ya Burnley ambayo juzi Jumanne usiku ilipanda hadi nafasi ya nne ambayo haijawahi kuifikia kwa miaka 42 iliyopita.

Kocha ya Wenger anapambana kukiweka kikosi chake kwenye nafasi nne za juu lakini suluhu hiyo imemuangusha.