‘Asilimia 50 wachezaji wanaingia uwanjani wamebeti’

Muktasari:

Akiri ni miongoni mwa watu wanaojishugulisha na kubeti jambo ambalo limekuwa utamaduni kwenye soka.

England. Mchezaji wa zamani England na Bunley amezungumzia suala la wachezaji kucheza kamali, huku akisema kwamba takribani asilimia 50 ya wachezaji huwa nawabeti kwenye mechi.

Alisema kwamba utamaduni wa kubeti kwa sasa imekuwa jambo la kawaida kwenye soka.

Hata hivyo, alishangazwa na kiwango hicho kikubwa kwa wchezaji kujihusisha na kucheza kamali kwenye mechi.

Aliongeza kuwa utamaduni wa kubeti kwa sasa umegeuka kuwa jambo la kawaida kwenye michezo.

Nyota huyo wa zamani alifungiwa kujishughulisha na masuala yoyote ya soka na adhabu yake itaisha Juni Mosi mwaka huu.

Mchezaji huyo anadai kwamba amecheza kamali mara 1,260 kwenye mechi mbalimbali kwa takribani miaka 10 kabla ya kufungiwa miezi 18 tangu mwezi Aprili baada ya kwenda kinyume na kanuni za soka.