He! Eti Cazorla ataka mkataba

Muktasari:

Mkataba wa Cazorla na Arsenal ya Profesa Arsene Wenger unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu.

Wakati kiungo Santi Cazorla akiwa na matumaini ya kurejea uwanjani muda mfupi ujao, Arsenal imeingia hofu kuhusu kumpa mkataba mpya.

Kiungo huyo fundi wa mpira wa Kihispaniola, yuko nje ya uwanja tangu Oktoba 2016 baada ya kufanyiwa

upasuaji wa kifundo cha mguu mara tisa, lakini Cazorla ameibuka na kudai anataka mkataba mpya.

Mkataba wa Cazorla na Arsenal ya Profesa Arsene Wenger unafikia tamati mwishoni mwa msimu huu, lakini mwenyewe anataka kumaliza soka lake klabuni hapo.