Eliuter Mpepo, ilikuwa kidogo tu aache soka

Muktasari:

  • Mshambuliaji wa zamani wa Tanzania Prisons, Eliuter Mpepo amesema kama sio uvumilivu leo hii asingekuwa mchezaji tegemeo kwenye kikosi cha Singida United kinachoshiriki Ligi Kuu Tanzania bara, Mpepo anasema mazingira aliyokutana nayo alipokuwa akiichezea Frinds Rangers ya Ligi daraja la kwanza yalimkomaza kisoka na kumjenga kwani alikumbana na chuki za viongozi iliyopelekea kutengenezea chuki hadi kwa mashabiki lakini alikomaa

Mshambuliaji wa zamani Tanzania Prisons, Eliuter Mpepo ambaye kwa sasa ni mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Singida United na ni kutokana na uwezo wake wa kuwasumbua mabeki, kufunga na kutengeneza mabao.

Eliuter (21) aliyekuwa akicheza na Mohammed Rashid ambaye naye ametimkia Simba, husimama kwenye eneo la mwisho la ushambuliaji la kikosi cha Singida na hiyo ndiyo msimu uliopita alifunga mabao manne na amengeneza mengine matano ya fasta.

Spoti Mikiki ilifanya mahojiano na mshambuliaji huyo ambaye ameizungumzia safari yake ya soka huku akizitaja changamoto ambazo amekutana nazo.

Kabla ya kutua Prisons na baadaye Singida, Eliuter alizichezea Kinyerezi United ambayo ilikuwa madaraja la nne, Friends Rangers na Mbeya Kwanza za daraja la Kwanza.

Hata hivyo Eliuter amesema hawezi kusahau mazingira aliyapitia akiwa Friends Rangers kwa kusema ni kama yalimkomaza kisoka.

“Ulifika muda mpaka nikaanza kuwaza kuachana na soka, nilivyojiunga na Friends kuna baadhi ya viongozi walikuwa hawanipendi kabisa hivyo walinitengenezea majungu kwa hata kupandikiza chuki kwa mashabiki.

“Walifanikiwa kiukweli maana kila nilipokuwa naingia nilikuwa nazomewa, hali ya kuzomewa nilishindwa kuimudu mpaka ikaanza kuathiri uwezo wangu wa kawaida wa uwanjani nilipiga moyo konde lakini niliushinda ule mtiani,” anasema Eliuter.

Pamoja na kuonekana kuwa mmoja wa washambuliaji hatari, Eliuter anasema hana tatizo wala mapenzi kati ya Simba na Yanga kama ukitokea upande wowote kumwitaji atakuwa tayari kuusikiliza.

“Nafanya kazi kokote bila ya kuhosifia chochote, naweza kucheza Simba na hata Yanga kama wakinihitaji. Tanzania Prisons walinipa nafasi nami nikacheza na sasa nipo Singida,” anasema.