Mchezaji wa Simba aangusha saini Mtibwa

Muktasari:

Luizio aliwahi kuitumikia Mtibwa kabla ya kutimkia Zambia katika timu ya Zesco United, kisha akatolewa kwa mkopo Simba na baadaye kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo moja kwa moja.

STRAIKA Juma Luizio aliyekuwa akiichezea Simba, amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumia Mtibwa Sugar msimu ujao.

Luizio aliwahi kuitumikia Mtibwa kabla ya kutimkia Zambia katika timu ya Zesco United, kisha akatolewa kwa mkopo Simba na baadaye kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo moja kwa moja.

Kurejea kwa mchezaji huyo katika kikosi cha Mtibwa, inakuwa ni mwendelezo kwa klabu hiyo kuwarejesha wachezaji wake pindi mambo yanapokuwa magumu katika timu nyingine.

Wachezaji wengine ambao waliwahi kutoka kurejea  ni Hussen Javu, Shabaan Nditi na Issa Rashid 'Baba Ubaya'.