Pogba amkosesha raha Dybala

Muktasari:

  • Kushuka kiwango kwa kiungo mahiri wa Ufaransa Paul Pogba, kumemstusha mchezaji mwenzake wa zamani wa Juventus, raia wa Argentina, Paulo Dybala, ambaye amesema ni jambo la kuhuzunisha kwa kilichomtokea huku akitamani kuona siku moja wanajumuika na kucheza katika timu moja.

Milan, Italia. Mshambuliaji mahiri wa Juventus raia wa Argentina, Paulo Dybala, ameelezea kusitikishwa na namna kiwango cha Paul Pogba kilivyomalizika ndani ya muda mchache tangu ajiunge na Manchester United.

Dybala alikipiga na Pogba pamoja kwa kipindi kifupi wakati wote wakiitumikia Juventus na kiungo huyo kutoka Ufaransa akapandiwa dau na kurejeshwa Old Trafford.

Akizungumza na mtandao wa klabu hiyo, Dybala alisema Pogba ni mmoja wa viungo bora duniani lakini anashangaa kuona kiwango chake kimeshuka.

Alisema katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya wiki mbili zilizopita licha ya United kuifunga Juventus mabao 2-1, lakini Pogba alicheza kwa kiwango cha chini tofauti na walivyomzoea.

“Nimesikitika kumshuhudia Pogba akicheza kwa kiwango cha chini, nilikuwa nikisikiwa akilaumiwa lakini sikujua kama ni kwa kiwango hiki ni mcheaji ambaye kila mmoja hapa lisikitika alipoondoka kutokana na ubora wake binafsi natamani na naamini ipo siku nitaunga naye tena,” alisema Dybala.

Alisema anamini ataungana tena na Pogba na kucheza katika timu moja inga wahajui ni lili na watakuana katika timu ipi ila alicho na matumaini ni kuwa watajacheza pamoja.