Mnigeria wa Njombe awaza mbali

Muktasari:

  • Tajudeen asema amesaini Njombe, baada ya kupata nafasi katika klabu hiyo, lakini anaamini kwamba safari yake ya soka bado inaendelea.

BEKI Ahmed Tajudeen, anayekipiga katika klabu ya Njombe Mji kutoka nchini Nigeria, amesema anataka kuhakikisha anafanya vizuri akiwa na klabu hiyo kisha ndio aonekane na vilabu vingine.

Tajudeen alisema anataka kuhakikisha Njombe Mji ifanye vizuri katika michezo iliyobaki kisha ndio ajiangalie upande wake.

"Huwezi ukasema unaondoka sasa hivi kama timu ikifanya vibaya, naangalia mbele sana lakini ni lazima timu ifanye vizuri katika michezo iliyobaki," alisema.

Tajudeen alisema amesaini Njombe, baada ya kupata nafasi katika klabu hiyo, lakini anaamini kwamba safari yake ya soka bado inaendelea.

"Naamini kabisa kwamba safari yangu ya soka bado inaendelea ndani na nje ya Tanzania, nilisaini Njombe kwa sababu hapa ndio nilipata nafasi ya kusajili baada ya kufanya majaribio na kufuzu," alisema.