Ronaldo kuifikia rekodi ya Messi leo

Muktasari:

Katika misimu mitatu Mreno huyo amekuwa katika kiwango cha juu

Paris, Ufaransa. Hafla ya kutolewa kwa tuzo ya mwanasoka bora wa Ulaya itafanyika leo Alhamis jijini na Paris, na mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo atakabidhiwa tuzo hiyo ya tano ya Ballon d'Or.

Hiyo itakuwa ni mara ya tano kwa Mreno huyo kupokea tuzo hiyo baada ya kufanya hivyo 2008, 2013, 2014 na 2016 -, atakapochukua tuzo ataifikia rekodi ya nyota wa  Barcelona, Lionel Messi.

Ronaldo atapewa tuzo hiyo inayoandaliwa na jarida la France Football, katika moja ya maeneo mazuri ya kupigia picha duniani katika mnara wa Eiffel jijini Paris.

Muonekana utakavyokuwa katika sherehe hiyo ya Ballon d'Or itafanana na inavyofanyika wakati wa utoaji wa tuzo ya washindi wa mashindano ya tenisi ya French Open inayofanyika karibu na mnara huo mashuhuru.

Mshambuliaji huyo wa Real, alifanikiwa kutwaa mataji mawili msimu uliopita  LaLiga na Ligi ya Mabingwa pamoja na kuisaidia timu yake kufuzu kwa Kombe la Dunia.