Friday, November 10, 2017

Messi,aomba,radhi kwa kumpotezea nyota wa Argentina

 

Moscow, Russia. Mshambuliaji Lionel Messi amemuomba radhi Muargentina mwenzake Sebastian Driussi wa FC Zenit baada ya kushindwa kumtambua alipopiga naye picha.

Kikosi cha Argentina kwa sasa kipo Russia tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi  ya wenyeji wa Kombe la Dunia ndipo tukio hilo lilipotokea katika hotel jijini Moscow.

"Najisikia vibaya kwa sababu sikumtambua, japokuwa namjua," alisema Messi.

"Wakati aliponiomba kupiga naye picha nilijua ni mmoja ya watu ambao wakaa kusubili ili kupiga picha, lakini nilimemuomba radhi baada ya tukio hilo."

Nahodha huyo wa Argentina alichukua uamuzi huo baada ya kuona Driussi ameituma picha hiyo katika ukurasa wake wa Instagram, na kumtumia ujumbe.

Driussi amejiunga na Zenit akitokea River Plate kwa gharama ya euros 15 milioni Julai mwaka huu.

 

-->