Sanchez aota makubwa Man Utd

Muktasari:

  • Sanchez amekuwa mchezaji wa kwanza anayelipwa mshahara mkubwa zaidi England

London, England. Alexis Sanchez amekamilisha uhamisho kwenda Manchester United kama ilivyokuwa kwa Henrikh Mkhitaryan aliyetimkia Arsenal.

Manchester United wametumia Twitter kumthibisha nyota huyo wa Chile kuwa mchezaji wa klabu hiyo kwa mshambuliaji huyo kupiga kinanda cha wimbo wa "Glory Glory Man United".

Wimbo huo mpya masikioni mwa mashabiki wa Man United, nyota huyo wa zamani wa Barcelona aliwambia viongozi wake kuwa: "Nimefurahi kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani.

"Nimekaa kwa miaka mitatu na nusu ya mafanikio ndani ya Arsenal na kunifanya mimi kubaki na kumbukumbu nzuri za klabu kubwa na mashabiki wake.

"Nafasi ya kucheza katika uwanja wenye historia na kufanya kazi chini ya Jose Mourinho ni jambo nililokuwa nalisubiri kwa muda mrefu.

"Najivunia kuwa mchezaji wa kwanza wa Chile kucheza Man United ni matumaini yangu nitawaonyesha mashabiki wote duniani kwanini klabu hii imepigana kunileta mimi hapa."

Naye kocha wa Manchester United, Mourinho aliongeza: "Alexis ni mmoja wa washambuliaji bora duniani ni mchezaji aliyetimia mwenye kipaji cha hali ya juu.

"Ningependa kumtakia kila kheri Henrikh katika maisha yake mpya katika klabu mpya naamini atafanya vizuri huko.

"Ni mchezaji ambaye hatutamsahau, hasa kutokana na mchango wake mkubwa uliochangia tukafanikiwa kutwaa ubingwa wa Europa Ligi."