Mashabiki wa Arsenal wagoma kwenda Uwanjani

Muktasari:

  • Arsenal msimu huu ipo katika mazingira magumu ya kumaliza katika nafasi nne za juu

London, England. Idadi ndogo ya mashabiki waliojitokeza katika mchezo wa Ligi Kuu England kati ya Arsenal dhidi ya Newcastle United, unaweza kumng’oa kocha Arsene Wenger.

Baadhi ya viti vya Uwanja wa Emirates vilibaki wazi baada ya mashabiki wa Arsenal kususa.

Kipigo cha mabao 2-1 ilichopata kutoka kwa Newcastle, kinamuweka katika mazingira magumu kocha huyo aliyeanza kuinoa Arsenal tangu mwaka 1996.

Mashabiki wa klabu hiyo kwa takribani mechi nne za ligi ilizocheza Arsenal walikuwa wachache uamuzi unaoweza kumgharimu Wenger majira ya kiangazi.

Licha ya kuendelea kupambana katika Kombe la Europa, Arsenal imejiweka katika nafasi ndogo ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya mwakani.