Lukaku, Fellaini matatani Man United

Muktasari:

Man United ilitwaa Kombe la FA, baada ya kuchapwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

London, England. Jose Mourinho amechukizwa na kitendo cha Romelu Lukaku na Marouane Fellaini kukacha mchezo wa fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea.

Man United ilitwaa Kombe la FA, baada ya kuchapwa bao 1-0 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye Uwanja wa Wembley.

Wakati Lukaku alidai ana jeraha la kifundo cha mguu, Fellaini alikosa mechi tatu kutokana na majeraha ya misuli kabla ya mchezo huo wa Jumamosi.

Hata hivyo, inadaiwa wachezaji hao wa timu ya Taifa ya Ubelgiji walidai ni wagonjwa na walihofia kuumia hatua ambayo ingewakosesha fainali za Kombe la Dunia zitakazoanza Juni 14 nchini Russia.

Chanzo cha karibu kilidokeza wachezaji hao walijumuishwa katika kikosi ambacho kingeivaa Chelsea katika mchezo huo.

Lukaku alimwambia Mourinho hayuko fiti akidai kupata jeraha la kifundo cha mguu.

“Mchezaji anapokwambia hayuko tayari kwa mchezo, swali linakuja unadhani atacheza kwa dakika ngapi, unaweza vipi kumshawishi mchezaji aliyekwambia hayuko tayari kucheza,” alisema Mourinho.

Mourinho alimkingia kifua libero Eric Bailly akidai anatambua hayuko fiti tangu alipofanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu na alikosa mchezo dhidi ya West Brom mwezi uliopita.

Mustakabali wa Fellaini Man United uko njia panda ya kushindwa kutia saini mkataba mpya huku kukiwa na taarifa za kutakiwa na kigogo cha soka Italia AC Milan.