Kane aondoa nuksi ya Agosti

STRAIKA matata na fundi wa kupasia nyavuni wa Tottenham, Harry Kane amemaliza ukame wa mabao akifunga bao lake la kwanza kwenye msimu mpya wa Ligi Kuu England.
Kane, ambaye aliibuka Mfungaji Bora kwenye fainali za Kombe la Dunia 2018 kule Russia, alipachika bao hilo kwenye ushindi wa 3-1 dhidi ya Fulham katika Uwanja wa Wembley.
Katika mchezo huo, mabao mengine ya Tottenham yalifungwa na Kieran Tripper na Lucas Moura. Huu ni ushindi wa pili kwa Spurs baada ya kuichapa Newcastle United manbao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza, ambao Kane alitoka kapa.
Hata hivyo, kufunga bao hilo sio ishu kubwa kwa Kane, lakini benchi la ufundi, mashabiki na wachezaji wenzake wamepatwa mzuka kutokana na staa huyo kuwa na gundu unapoingia mwezi huu wa Agosti.
Rekodi zinaonyesha kuwa, Kane amekuwa akikumbana na wakati mgumu wa kupasia nyavuni kila unapofika mwezi kama huu hivyo, bao hilo limepokewa kwa furaha kwelikweli klabuni kwake.

KAMATA HII

Marcos Alonso
Beki wa Chelsea, Marcos Alonso amehusika kwenye mabao 20 katika Ligi Kuu England tangu aliposajiliwa mwaka 2016. Amefunga mabao 14 na kutoa pasi za mabao sita, ambapo hakuna beki mwingine aliyefanya hivyo.

Cristiano Ronaldo
Supastaa mpya wa Juventus, Cristiano Ronaldo jana alianza kuichezea timu yake mechi ya kwanza ya Serie A huku wakichomoza na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Chievo ugenini. Hata hivyo, kwenye mchezo huo, Ronaldo amemaliza dakika 90 bila kufunga bao.