APR, Rayon kurudiwa kesho

Muktasari:

  • Mchezo utaanzia dakika ya 63 sekunde ya 42 ambayo ilisimamishiwa mechi hiyo jana. Katika muda huo Rayon Sport ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya APR.

Kigali, Rwanda. Shirikisho la Soka la Rwanda (FERWAFA) limesema mchezo kati ya APR na Rayon Sport ulivunjika jana dakika ya 63 kwa sababu ya kukatika umeme uwanjani,utarudiwa kuchezwa kesho.

Mchezo utaanzia dakika ya 63 sekunde ya 42 ambayo ilisimamishiwa mechi hiyo jana. Katika muda huo Rayon Sport ilikuwa mbele kwa mabao 2-0 dhidi ya APR.

Katika mchezo huo wa kesho, APR itaingia uwanjani na wachezaji 10 baada ya mmoja kupewa kadi nyekundu.