Friday, November 10, 2017

Messi azindua mpira mpya kwa hat-trick Urusi

 

Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) limeutangaza mpira mpya wa Adidas Telstar 18, ndiyo utakaotumika katika Kombe la Dunia 2018 Russia.

Mpira huo umetengenezwa  kwa kiwango ambacho kimewahi kutumika  kwenye Kombe la Dunia mwaka 1970.

Taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa Adidas ilieleza kwamba mpira huo uliotangazwa ndio utakaotumika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Urusi mwakani.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa aina hiyo ya mpira imewahi kuchechezwa na wakongwe wa soka kama vile Pelé, Gerd Müller, Giacinto Facchetti, Pedro Rocha na Bobby Moore.

Mabao matatu ya Lionel Messi wakati wa mechi ya Argentina dhidi ya Ecuador  ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 ilikuwa ni sehemu y uzinduzi wa mpira huo kwenye sherehe ya ufunguzi iliyofanyika Moscow.

Nyota huyo wa Barcelona, alisema imekuwa jambo la bahati kwake kuuona mpira huo na ameuchezea pia akisisita kwamba una viwango.

Messi alisema kinachovutia zaidi kwenye mpira huo ni muundo mpya uliotengenezwa pamoja na rangi na vitu vingine vinavyoupendezesha.

-->