Alliance watakuwa kusajili wakongwe watano

Muktasari:

Timu hiyo ya Shule ya kukuzia vipaji ni moja ya timu sita za Ligi Daraja la Kwanza zilizopanda daraja msimu huu

Mwanza. Beki wa zamani wa Toto Africans,Victor Nyalila ameipa neno Alliance FC akiwataka kusajili wachezaji watano wenye uzoefu ili kuwafanya kuwa bora zaidi katika msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Nyalila alisema ili Alliance iwe moto msimu ujao wanatakiwa kusajili wachezaji watano wazoefu wa Ligi Kuu ambao watasaidiana na vijana waliopo kikosini hapo.

Alisema timu hiyo inatakiwa kusajili beki wa kati, washambuliaji wawili, kiungo mkabaji pamoja na kipa mmoja ambapo alisema wachezaji hao wanaweza kuwa wa hapa bongo au wa kutoka nje ya nchi.

“Alliance wana timu nzuri, lakini wanatakiwa kuongeza wachezaji wazoefu kwani Ligi Kuu ina mambo mengi hivyo ni lazima wawepo wakongwe ambao watawaongoza vijana ndani ya kikosi,” alisema Nyalila.

Alisema kama Alliance wakifanya hivyo watakuwa na kikosi bora ambacho Simba na Yanga zitakuwa na kazi nzito msimu ujao.

Hata hivyo; beki huyo aliwataka mashabiki wa soka wa jijini hapa kuipa sapoti Alliance katika mechi zake za Ligi Kuu msimu ujao.