Argentina, Brazil waanika vikosi vyao

Muktasari:

  • Tofauti na Argentina, ambayo imetangaza majina ya nyota 35, ambao itawafanyia mchujo na kubakisha watakaokwenda Urusi kwa ajili ya fainali hizo, Kocha wa Brazil, Tite ametangaza orodha kamili ya wachezaji 23 ambao moja kwa moja wameshajihakikishia nafasi ya kuiwakilisha Brazil kwenye mashindano hayo.

Wakati Kocha wa timu ya Taifa ya England, Gareth Southgate akitarajiwa kutangaza kikosi chake kwa ajili ya maandalizi fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Urusi mwezi ujao, makocha wa Argentina na Brazil wametangaza mapema majina ya nyota waliomo kwenye vikosi vyao kuelekea fainali hizo.

Tofauti na Argentina, ambayo imetangaza majina ya nyota 35, ambao itawafanyia mchujo na kubakisha watakaokwenda Urusi kwa ajili ya fainali hizo, Kocha wa Brazil, Tite ametangaza orodha kamili ya wachezaji 23 ambao moja kwa moja wameshajihakikishia nafasi ya kuiwakilisha Brazil kwenye mashindano hayo.

Katika kikosi hicho cha Brazil kuna kundi la nyota sita wanaocheza kwenye Ligi Kuu Engand lakini pia Tite amejumuisha nyota saba, ambao walishiriki kwenye Fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini kwao mwaka 2014 ambapo walipata kipigo cha aibu cha mabao 7-1 kutoka kwa Ujerumani kwenye mechi ya nusu fainali.

Kikosi hicho cha Brazil kinaundwa na makipa Allison, Ederson, Cassio huku mabeki wakiwa ni Danilo, Fagner, Marcelo, Filipe Luis, Thiago Silva, Marquinhos, Miranda na Pedro Geromel

Viungo wanaounda kikosi hicho ni Casemiro, Fernandinho, Paulinho, Fred, Renato Augusto, Philippe Coutinho, Douglas Costa na Willian huku washambuliaji wakiwa ni Neymar, Taison, Gabriel Jesus na Roberto Firmino.

Katika kikosi cha Argentina, wachezaji walioitwa ni makipa Sergio Romero, Nahuel Guzman, Willy Caballero, Franco Armani, mabeki wakiwa ni Gabriel Mercado, Javier Mascherano, Nicolas Otamendi, Federico Fazio, Nicolas Tagliafico, Marcos Rojo, Marcos Acuna, Ramiro Funes Mori, Cristian Ansaldi, Eduardo Salvio, German Pezzella.

Kocha Jorge Sampaoli amewaita viungo Angel Di Maria, Ever Banega, Lucas Biglia, Manuel Lanzini, Gio Lo Celso, Ricardo Centurion, Guido Pizarro, Leandro Paredes, Maximiliano Meza, Enzo Perez, Pablo Perez, Rodrigo Battaglia na Cristian Pavon wakati washambuliaji ni Lionel Messi, Sergio Aguero, Gonzalo Higuain, Paulo Dybala, Mauro Icardi, Lautaro Martinez na Diego Perotti.