Arsenal yaiotea AC Milan 3-1

Muktasari:

  • Welbeck afunga mabao mawili na kupunguza presha kwa kocha Arsene.

Mabao ya Danny Welbeck na Granit yameipeleka Arsenal hatua ya robo fainali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuvuka hatua hiyo kwa jumla ya mabao (5-1) kwenye mashindano ya Ligi ya Europa.

Welbeck alifunga mabao mawili na kupunguza presha kwa kocha Arsene Wenger ambaye amekuwa akiandamwa kutakiwa kujiuzulu.

Arsenal walionekana kutawala mchezo katika vipindi vyote viwili jambo lililowapa mwanya wa kufanya vyema kwenye mchezo huo muhimu kwa kikosi cha Wenger.

Arsenal ndiyo timu pekee ya England inayowakilisha Ligi ya Europa huku Manchester United, Chelsea, Tottenham zikiondolewa Ligi ya Mabingwa Ulaya, hata hivyo Man City na Liverpool zimebaki kwenye mashindano hayo makubwa barani Ulaya.