Kipigo cha Atletico shangwe Barcelona

Muktasari:

Timu hizo Barcelona na Atletico zimetofautiana kwa pointi 12 kwa sasa

Barcelona, Hispania. Barcelona sasa wanahitaji kushinda mechi mmoja kutwaa ubingwa kwa mara 25 msimu huu baada ya Atletico Madrid kufungwa 2-0 na Real Sociedad.

Vijana wa Diego Simeone wanaoshika nafasi ya pili baada ya kuruhusu bao la Willian Jose aliyemalizia kazi nzuri ya nyota wa zamani wa Manchester United, Adnan Januzaj.

Juanmi aliyeingia akitokea benchi alifunga bao la pili kufanya matokeo kuwa 2-0, katika dakika za mwisho za mchezo huo.

Barcelona watatwaa ubingwa wa La Liga iwapo watashinda dhidi ya Deportivo La Coruna katika mchezo Aprili 29.

Barca iliyomaliza nafasi ya pili msimu uliopita nyuma ya watani zake wa jadi Real Madrid.

Atletico inayoshika nafasi ya pili ipo nyuma kwa pointi 12 kwa Barcelona ikiwa imebakia michezo mitano, watasafiri kuifuata Arsenal katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya Europa Ligi utakaopigwa Aprili 26.