Azam FC yafufua matumaini kutetea ubingwa Kombe la Kagame

Muktasari:

  • Awali Azam na Gor Mahia zilimaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana kisha zikaongezwa dakika 30 ambako yalipatika mabao hayo mawili ya Azam na kuifanya kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wake.

Azam FC yafufua matumaini kutetea ubingwa Kombe la Kagame

Timu ya Azam imefuzu kucheza fainali ya Kombe la Kagame 2018 baada ya kuifunga Gor Mahia mabao 2-0 katika mechi ya kwanza ya nusu fainali kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Awali Azam na Gor Mahia zilimaliza dakika 90 zikiwa hazijafungana kisha zikaongezwa dakika 30 ambako yalipatika mabao hayo mawili ya Azam na kuifanya kufufua matumaini ya kutetea ubingwa wake.

Hata hivyo Azam ilishuka dimbani bila straika wake, Shaban Chilunda baada ya klabu ya Tenerife ya Hispania kukamilisha baadhi ya vitu ambavyo vilikuwa vimesalia katika mkataba wake.

Chilunda alisaini mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Pili nchini Hispania, huku akiwa ni mchezaji wa pili baada ya Farid Mussa kwenda awali katika timu ya vijana katika klabu hiyo hiyohiyo.

Kikosi cha Azam kilichoivaa Gor Mahia  ni Razack Abarola, Nicco Wadada, Bruce Kangwa, Abdallah Kheri, Aggrey Morris,Mudathir Yahya, Joseph Mahundi, Frank Domayo, Ditram Nchimbi,Salum Aboubacary na Ramadhan Singano.