Griezmann kutua Barca

Tuesday November 14 2017

 

Barcelona, Hispania.Barcelona imefikia makubaliano ya awali ya kutaka kumsaini mshambuliaji Antoine Griezmann, kwa mujibu wa taarifa kutoka Ufaransa.

Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid amekuwa na msimu mbaya akiwa amefunga mabao mawili tu hadi sasa katika La Liga.

Pamoja na kuwepo kwa taarifa za Manchester United kwa muda mrefu, lakini ujio wa Barcelona umeongeza changamoto ya kuisaka saini ya Mfaransa huyo.

Gazeti la Le 10 Sport lilidai kuwa miamba ya Catalans imepiga hatua kubwa katika kuisaka saini ya Griezmann.

Mfaransa huyo alitegewa angejiunga na Man United msimu huu, lakini uamuzi wa Fifa kuzuia uhamisho wa  Atletico ulikwamisha uhamisho huo.

Griezmann alisaini mkataba mpya uliongeza thamani yake mara mbili kutoka pauni 85milioni hadi pauni170m  endapo atauzwa.

Huku uwezo wa Luis Suarez katika kuzifumania nyavu ukiwa umeshuka, jambo linalowafanya Barcelona kurudi sokoni kutafuta mshambuliaji mwingine.

 

 

Advertisement