Beki wa Liverpool akoleza moto mbio za ubingwa

Muktasari:

  • Beki wa timu ya Liverpool, Virgil van Dijk, amesema kuwa anaamini timu hiyo itachuana na Manchester City katika mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England hadi mwisho wa msimu na kamwe haitakata tamaa.

Liverpool, England. beki wa Liverpool raia wa Uholanzi, Virgil van Dijk, amesema anaamini timu hiyo itachuana na Manchester City mpaka mwisho katika mbio za ubingwa wa England msimu huu.

Mlinzi huyo ameyasema hayo baada ya Man City kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Man United timu iliyodhaniwa huenda ingeisimamisha Man City inayopigania kutetea taji hilo.

Man City, Liver pamoja na Chelsea ndizo pekee ambazo hajizapoteza mchezo katika Ligi msimu huu na Van Dijk anaamini City haitaweza kuendeleza ubabe wake kwa timu zote.

Alisema kikosi hicho cha kocha Pep Guardiola, hakina ubora zaidi kuzizidi klabu zingine hivyo anaamini uwezekano wa kuchuana nayo na kuipukua katika mbio za ubingwa upo.

“Mimi siamini kwamba Man City pekee ndiyo timu yenye nafasi ya kutwaa ubingwa msimu huu, naamini Liverpool inaweza kufanya hivyo n ahata timu zingine ikiwa tulitoka nao sare na wakabanwa pia na Wolverhampton Wanderers tutashindwaje kuchuana nal,” alihoji.

Timu hizo zinatofautina kwa pointi mbili City ikiendelea kuongoza katika mbio za ubingwa wa msiomu huu huku pia ikiwa na hazia kubwa ya mabao kwani hadi sasa imefunga mabao 36 yakiwa ni 13 zaidi ya waliyonayo Liver.

“Msimu bado sana kwa kweli sidhani kama ni sahihi kuanza kusema eti City imeshajidhihirisha kuwa ndiyo bingwa mtarajiwa wa Ligi kwa msimu huu, sisi pia bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa,” alisema.

Alijitapa kwamba hawatarudia makossa waliyoyafanya katika msimu uliopita ambao walichuana vilivyo na Man City lakini wakalegaza Kamba dakika za mwisho na kuiachia timu hiyo kutwaa ubingwa.