Bocco atoboa mbinu za ushindi Simba kwa Al Masri

Muktasari:

  • Bocco alisema endapo watapata bao la mapema awamu hii watalilinda ili liweze kudumu

NAHODHA wa Simba, John Bocco amesema wameona makosa waliyofanya kwenye mechi ya awali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry na tayari wameyafanyia kazi ili waweze kufanya vizuri kwenye mechi ya kesho Jumamosi usiku.

Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza jijini Dar es Salaam hivyo inahitaji ushindi wa aina yoyote ili kusonga mbele.

Bocco alisema endapo watapata bao la mapema awamu hii watalilinda ili liweze kudumu tofauti na mchezo wa awali ambapo walifunga bao likarudishwa muda huo huo.

"Tumejifunza kwa makosa hayo hivyo hatutakubali yajirudie kwenye mechi hii. Tunakwenda kupambana na tuna imani ya kushinda," alisema Bocco.