Bocco ajiengua Taifa Stars

Muktasari:

  • Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'tryagain' alisema; "Bocco bado hayuko fiti, akirejea Dar tutampa matibabu zaidi

STRAIKA wa Simba, John Bocco amejiengua kwenye kikosi cha Taifa Stars kutokana na maumivu ya mguu.

Bocco alirejeshwa kwenye kikosi cha timu hiyo ya Taifa kitakachocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Algeria na DR Congo lakini habari mbaya ni kwamba hataweza kuitumikia timu hiyo.

Akizungumza na Mwanaspoti mjini hapa,  Bocco alisema ameomba ruhusa maalumu kwani bado anajisikia maumivu hivyo anataka kupatiwa matibabu zaidi.

Naye Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'tryagain' alisema; "Bocco bado hayuko fiti, akirejea Dar tutampa matibabu zaidi hivyo tumeomba asiende timu ya Taifa."