Chelsea yamnyatia Anthony Martial

Muktasari:

  • Chelsea yenye maskani yake Stamford Bridge, ipo kwenye presha kubwa kutoka kwa Real Madrid inayomhutaji Hazard na Barcelona inayohaha kumsajili Willian.

London, England. Klabu ya Chelsea inayopambana kuwabakisha viungo wake mahiri Eden Hazard na Willian, imeanza kusaka wachezaji watakaochukua nafasi zao.

Chelsea yenye maskani yake Stamford Bridge, ipo kwenye presha kubwa kutoka kwa Real Madrid inayomhutaji Hazard na Barcelona inayohaha kumsajili Willian.

Baada ya kuona ugumu wa kuwazuia wachezaji hao, Chelsea imeamza kusaka warithi na inamuona mmoja wapo ni Anthony Martial, 22, ambaye anaonekana kutokua na nafasi katika kikosi cha Manchester United tangu ianze kunolewa na Old Trafford.

Hata hivyo Chelsea watalazimika kuchuana na Juventus inayojipanga upya ambayo tayari imemsajili Cristiano Ronaldo kutoka Real Madrid katika usajili uliowastusha wengi.

United haitazamiwi kumuchia kirahisi mchezaji huyo kwenda Chelsea ambayo itakuwa mshindani wake katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England.

Chelsea inasemakana imechoshwa na ofa za Barcelona na sasa iko tayari kumuachia Willian kwa adan ya Pauni 65 milioni.