Thursday, September 21, 2017

Costa akaribia Atletico Madrid

 

STAA wa Chelsea, Diego Costa anakaribia kabisa kutua katika klabu yake ya zamani ya Atletico Madrid na anaweza kupimwa afya ndani ya saa chache zijazo kwa ajili ya kukamilisha uhamisho huo ambao unaweza kuigharimu Atletico kiasi cha Pauni 53 milioni.

Costa anatazamiwa kutambulishwa ndani ya siku chache zijazo ingawa hatazamiwi kukipiga Atletico mpaka Januari mwakani kufuatia timu hiyo kufungiwa kununua wachezaji kwa sasa na atakuwa huru pindi dirisha la Januari litakapofunguliwa.

Costa anaweza kuwa jukwaani kama mchezaji mpya wa Atletico katika pambano dhidi ya Chelsea Jumatano ijayo michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya akiwa amerejea klabuni hapo baada ya kununuliwa na Chelsea katika dirisha la majira ya joto mwaka 2014.

-->