Cristiano Ronaldo atwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia

Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristian Ronaldo

Muktasari:

Ronaldo (31), ambaye ni raia wa Ureno aliwapiku kina Lionel Messi wa Barcelona na Antonie Griezmann wa Klabu ya Atletico Madrid katika hafla iliyofanyika jana mjini Zurich, Uswisi.

Zurich, Uswisi. Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristian Ronaldo ametangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Ronaldo (31), ambaye ni raia wa Ureno aliwapiku kina Lionel Messi wa Barcelona na Antonie Griezmann wa Klabu ya Atletico Madrid katika hafla iliyofanyika jana mjini Zurich, Uswisi.

Desemba mwaka jana, Ronaldo aliibuka mshindi wa tuzo ya Ballon d’or baada ya kuiwezesha klabu yake kuibuka na ubingwa wa Klabu Bingwa Ulaya na kunyakua kombe la Euro akiwa na timu yake ya Taifa ya Ureno.

Katika hafla ya jana, Meneja wa Klabu ya Leicester City, Claudio Ranieri alitangazwa kuwa kocha bora wa mwaka kwa upande wa wanaume .

Katika ukurasa wake wa facebook, Ronaldo aliandika amefurahishwa kushinda tuzo hiyo ya Fifa kwa mara ya kwanza, “2016 ulikuwa mwaka wa ndoto ambayo  isingewezekana bila msaada wa wachezaji wenzangu na kocha. Pia, nawashukuru wote walionisaidia kila siku. Asante kwa kila mmoja wao.”