Dalali asifu uongozi wa Rais wa muda Simba

Muktasari:

  • Dalali aliyasema hayo baada ya Simba kupata matokeo ya kuilaza Mwadui mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayoendelea.

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali amesema kuwa mafanikio ya Simba kwa sasa ni kutokana na Rais wa muda wa sasa, Salim Abdallah kuwaunganisha pamoja watu wote na ndiyo maana Simba inapata mafanikio.

Dalali aliyasema hayo baada ya Simba kupata matokeo ya kuilaza Mwadui mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu Bara inayoendelea.

"Simba hii ina mafanikiop ni kutokanan na umoja. Huyu Rais wa muda habagui, ameunganisha watu wote na wote Simba wana furaha ya mafanikio, Simba ni bingwa mwaka huu.

"Hatutaki kubahatisha, lengo ni kuona Simba inatwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu na hicho ndicho wanachotaka wanachama wa Simba," alisema Dalali.