Wednesday, September 13, 2017

Dar yapewa mipira 300

 

By Charles Abel

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), leo Jumatano limetoa mipira 300 kwa Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mpango wa kuinua soka la vijana.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TFF anayewakilisha Kanda ya Dar es Salaam, Lameck Nyambaya alisema shirikisho litahakikisha mipira hiyo inatumika vizuri ili kutimiza lengo.
"Tunaigawa mipira hii kwa vituo vya soka na mimi binafsi nitahakikisha kunakuwa na matumizi sahihi na sio vinginevyo.
Kutokana na ukubwa wa jijini hili, nilimuomba Rais wa TFF atupatie mipira 200 ambayo ametupatia na mimi mwenyewe nitaongeza mipira 100," alisema Nyambaya.
Hivi karibuni, TFF ilianzisha kampeni ya kugawa jumla ya mipira 3,100 ya soka nchi nzima kwa ajili ya soka la vijana.

-->